Diamond anaongozwa na tamaa. Anatamani kufika mahali pakubwa zaidi duniani. Na hiyo ndiyo tofauti kubwa iliyopo kati yake na wanamuziki wengine wa daraja lake Tanzania.
Tamaa ya Diamond inamwelekeza kutumia fedha nyingi kuwekeza. Na uwekezaji huo umekuwa ukimpa matokeo makubwa. Huwezi kummudu Ne-Yo, kumweka Tanzania na kurekodi naye wimbo kisha kufanya naye video Marekani bila uwekezaji.
Kuhusu tamaa bila shaka kila mwanamuziki anayo. Hata hivyo tofauti iliyopo kati ya Diamond na wanamuziki wengine ni jinsi ambavyo anashughulikia tamaa zake kuwa kweli. Anafanya uwekezaji mzuri kupata matokeo anayohitaji.
Kufanya ngoma na P-Square kisha kwenda kuwagharamia kukaa nao Afrika Kusini kurekodi video ya Kidogo, inahitaji uwekezaji.
Tofauti ya Diamond na wanamuziki wengine inaonekana pale kila mmoja anaposhika fedha na kutumia. Diamond hutumia fedha anazopata kuwekeza zaidi kwenye muziki, wakati wengine huzitumbua kwa starehe au kufanya uwekezaji mwingine nje ya muziki.
Wahenga walishatwambia kuwa mtu huvuna anachopanda. Diamond anaonekana ni mwanamuziki mwenye thamani kubwa Tanzania na Afrika yote kwa sasa, sababu ni uwekezaji ambao anaufanya kwenye muziki wake.
Hili ni somo ambalo wanamuziki wengine wanatakiwa kulichukua. Wengi ni wazuri na ubora wao studio ni mkubwa kuliko Diamond. Hata hivyo, Diamond anawashinda kwa ubora nje ya studio.
Narudia kwa msisitizo; Wanamuziki wengi Tanzania ni wazuri na wenye thamani kubwa studio kuliko Diamond. Wanaimba vizuri kuliko Diamond. Hata hivyo, Diamond ana thamani kubwa nje ya studio.
Thamani ya Diamond nje ya studio ni jinsi ambavyo hutafsiri tamaa zake za kufanikiwa kwa kuwekeza ili kupata matokeo anayohitaji. Kupata matokeo kama ya Diamond lazima uwekeze.
Ifahamike kuwa kuwekeza ni kujinyima. Kuna vitu utatamani zaidi lakini utalazimika kuviacha ili kuwekeza katika matokeo makubwa ambayo mtu unakuwa unayaota. Diamond alijinyima kwa ajili kuwekeza ndiyo maana anapata tunayoyaona.
Ndimi Luqman MALOTO
TRA NA WASHAURI WA KODI 100 WAJADILIANA SHERIA ZA KODI
Mkurugenzi wa Divisheni ya Mashauri ya Madai na Usuluhishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Obadia Kameya akifungua semina ya elimu ya sheria za kodi iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ambapo washauri wa masuala ya kodi walijadili namna ya utekelezaji wa mabadiliko mbalimbali katika sheria za kodi nchini.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akizungumza wakati wa semina ya kujadili namna bora ya utekelezaji wa mabadiliko katika sheria za kodi iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania.
Washauri wa masuala ya Kodi (Tax Consultants) walioshiriki katika semina ya kujadili namna bora ya utekelezaji wa mabadiliko ya sheria za kodi nchini iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na kampuni ya ushauri wa masuala ya kodi ya Hanif Habib & Co.Semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Benki Kuu jijini dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Divisheni ya Mashauri ya Madai na Usuluhishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Obadia Kameya akiwa katika picha ya pamoja na Washauri wa masuala ya kodi (Tax Consultants) baada ya semina ya majadiliano ya namna bora ya utekelezaji wa mabadiliko na maboresho katika sheria za kodi nchini kuisha.Semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa benki kuu ya Tanzania.
LUIS ENRIQUE ABWAGA MANYANGA BARCELONA
Luis Enrique anaamua kupumzika Barcelona baada ya miaka mitatu ya kufanya kazi klabu hiuyo ya Katalunya
Mholanzi huyo ataondoka miaka 25 baada ya ushindi wake wa Wembley kuipa Barcelona taji la kwanza kabisa la Ulaya.
Imekuwa siri ya wazi kwamba Enrique hataongeza mkataba mwishoni mwa msimu na ataondoka.
Uamuzi wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 46 kutangaza sasa kuondoka kwake, ni kama kuwaambia wachezaji wake wajitume kumaliza msimu vizuri ili wagane kwa furaha.
"Nitamalizia mkutano huu na Waandishi wa Habari kwa namna tofauti, nataka kutangaza kwamba sitaendelea kuwa kocha wa Barcelona. Nataka kuishukuru klabu kwa imani yao yote waliyoonyesha kwangu. Hiyo imekuwa miaka mitatu ya kutosahaulika,"alisema jana baada ya ushindi wa 6-1 dhidi ya Sporting Gijon jana.
Ushindi huo umeirejesha Barca kileleni mwa La Liga, ikifikisha pointi 57 baada ya mechi 25 na kuashushia nafasi ya pili, Real Madrid yenye pointi 56 za mechi 24 sasa baada ya sare ya 3-3 na Las Palmas jana.
No comments:
Post a Comment