KATIBU Mkuu Wizara ya Maliasili na Utaliii Profesa Eliamani Sedoyeka amezindua magari tisa aina ya Land cruiser na malori mawili, mitambo na vyombo vingine vya usafiri mali ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) vyenye jumla ya thamani ya Sh.bilioni 5.6.
Akizungumza baada ya kuzindua magari hayo jana, Desemba 14 mwaka 2022 ,Profesa Sedoyeka amesema magari hayo ni muhimu katika kutimiza malengo yao ya kulinda na kuhifadhi rasilimali za Misitu nchini .
"Nadhani wote tunatambua sio Tanzania pekee yake bali duniani kote tunapita kipindi kigumu cha mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha uzalishaji mkubwa wa hewa ukaa, hivyo ili kukabiliana na changamoto hizo moja ni kupunguza uharibifu wa mazingira na jinsi ya kutibu ni kupanda miti.
"Hivyo TFS ni ya kimkakati kwa Wizara yetu ya Maliasili na Utaliii na Taifa kwa ujumla kuhakikisha tunaboresha ,tunatibu yale maeneo yote ambayo miti imeondoka kwa kupanda miti mipya tukitambua miti ni rasilimali kwa maana ya kwamba utatengeneza ajira,utauza mbao ,utauza kuni na mazao mengine yatokanayo na miti,"amesema Profesa Sedoyeka.
Aidha ametumia nafasi hiyo kuipongesa TFS kwani katika Wizara imekuwaya mfano na tangu kuanzishwa kwake mpaka leo imekuwa imekuwa ikitimiza majukumu yake ya msingi vizuri na hilo wanajivunia
"Nitumie nafasi hii kusishukuru Serikali ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuipitisha bajeti iliyotuwezesha kununua magari haya kwani hivi sasa tungekuwa tunazungumzia habari ya kupewa msaada lakini bajeti ya TFS imewezesha kupatikana kwa bagari hayo .
Pia amesema Wizara kupitia TFS itaendelea kuhakikisha rasilimali ya mistu inalindwa kwa nguvu zote huku akifafanua Wakala huo ni jeshi na kazi ya sehemu ya jeshi ni kulinda.Pia TFS ni wataalamu katika kupanda, kutengeneza misitu na kuitunzaa.
"Na raslimali hii ya misitu inapokuwa nzuri tunafaidika wote kama nchi kwa wale wanaonufaika moja kwa moja kwa maana ya kupata mbao ama mazao ya misitu lakini misitu ikiwa kwenye hali nzuri tunapata mvua za kutosha ambazo zinatuwezesha kupata maji ya kuzalisha umeme, shughuli za kilimo pamoja na uendeshaji wa shughuli nyingine za kiuchumi,"amesema.
Katika hatua nyingine Profesa Sadoyeka amesema katika majukumu ya msingi ya TFS, Wizara itaendelea kuunga mkono na mbali ya kuzindua magari hayo watakuwa na kikao kazi ambacho kitajadili masuala mbalimbali yakiwemo ya kujipanga kwa ajili ya mwaka ujao wa fedha.
Amefafanua kwa kuhakikisha Wakala huo unapata raslimali zote ambazo zinazihitaji ili iendelee kutimiza malengo yake huku akitumia nafasi hiyo kueleza katika kukabiliana na majanga ya moto kwenye misitu Wizara Iko kwenye mchakato wa kununua vifaa vya kisasa vya kuzimia moto ambavyo vitatumika kwa ushirikiano wa taasisi, Wakala na hifadhi zote za Taifa zilizopo nchini.
Awali Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) Profesa Dos Santos Silayo amesema ili kuwezesha vituo vyao kufanya kazi kwa ufanisi wamekuwa wakitenga fedha za ununuzi magari, pikipiki, mitambo na vyombo vya usafiri majini kama boti za aina mbali mbali na zenye uwezo tofauti...
.jpeg)
No comments:
Post a Comment