.jpg)
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na
wananchi kuhusu uvamizi katika Msitu wa Kuni Wilaya ya Mvomero mkoani
Morogoro wakati wa ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta.
Baadhi
ya wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.
Mary Masanja (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu
uvamizi katika Msitu wa Kuni Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wakati wa
ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta.
Kutoka
kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Fatma Mwassa, Waziri wa Mifugo
na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki, Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Maryprisca
Mahundi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb)
wakati wa mkutano na wananchi katika Msitu wa Kuni Wilaya ya Mvomero
Mkoani Morogoro ikiwa ni ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta ya
kutatua migogoro ya ardhi mkoani humo.
NA MWANDISHI WETU
NAIBU
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewataka
wananchi waliovamia Msitu wa Kuni na kuanzisha shughuli za ujenzi wa
nyumba, kuacha mara moja na kuondoka katika eneo hilo la hifadhi .
Ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi katika Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.
“Sasa
tunachowaomba kwanza kusimamisha ujenzi kwenye eneo la msitu ,pili
tutaangalia wale ambao wamejimilikisha maeneo makubwa lazima tuyagawe
kwa sababu wote ni wavamizi” amesisitiza Mhe. Masanja.
Amesema
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
kwa huruma yake aliruhusu eneo la msitu limegwe jumla ya hekta 2000
ambazo zitagawiwa kwa wananchi lakini wananchi wameendelea kulivamia
eneo la msitu.
“Mwaka
jana tukaelekeza wananchi wapangwe kwenye hekta elfu 2000 na hiyo ni
huruma ya Mheshimiwa Rais Samia kwanza naomba tumpongeze mama yetu ana
huruma kwa sababu ilikuwa muondolewe lakini akasema hapana hawa ni
wananchi wangu wapangwe” Mhe. Masanja amefafanua.
Ameweka
bayana kuwa wananchi waliomo kwenye hekta elfu 2000 zilzizogawiwa wako
kihalali na watapimiwa ardhi na kupewa hati zao lakini waliovamia
wanapaswa kuondoka katika eneo hilo.
Katika
hatua nyingine , Naibu Waziri Masanja amewaasa wananchi wa Kijiji cha
Ngombo Wilayani Malinyi, kuhifadhi mazingira na kuacha tabia ya kukata
miti hovyo kwa faida ya kizazi cha sasa na cha baadae.
No comments:
Post a Comment