WAZIRI wa Maji Mhe Jumaa Aweso amefika, kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maji ya muda mfupi Wilaya ya Kasulu jimbo la Kasulu Mjini, akizungumza katika eneo la Mradi kata Kumunyika katika mradi wa Maji Mudandya na Mradi wa Maji Juhudi ikiwa ni sehemu ya ziara yake kata na maeneo mbalimbali Kasulu mjini ameonesha kutoridhishwa na kazi iliofanyika pamoja na matumizi ya fedha sambamba na kuchelewa kwa kukamilika kwa mradi.
Pia, Waziri Aweso ametekeleza agizo la Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango alilotoa tarehe 05 Julai 2023 kufika Kasulu mjini na kutatua changamoto kwa hatua za muda mfupi wakati Mradi mkubwa ukiendelea kutekelezwa.
Katika ziara yake, Waziri Aweso
amesisitiza kazi kufanyika ndani ya miezi mitatu wananchi wapate maji kwa
mikakati ya muda mfupi wakati Utekelezaji wa mradi mkubwa wa Maji Miji 28
Kasulu ukiendelea.
Aidha Waziri Aweso ametoa wito kwa wahandisi wa maji
kuhakikisha wanatekeleza miradi kwa ufanisi na kwa wakati wakizingatia matumizi
sahihi ya fedha.
Waziri Aweso ameweka wazi maelekezo ya kukaa pembeni kwa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Kasulu Mjini Eng Riziki Nyamtega na kuahidi
kuleta uongozi mpya wilayani hapo na kuisuka upya Mamlaka hiyo ya Maji.
Akizungumza na wanachi ameahidi kuleta Milion 500
kuongeza nguvu katika kufanikisha miradi ya muda mfupi.
Katika kipindi cha Utekelezaji
wa maagizo hayo Mhe Aweso ameelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji
Nzega Eng Athumani kilundumya kuisimamia Mamlaka hii katika kipindi cha
Utekelezaji wa maagizo yake akiendelea kuiunda Mamlaka.
No comments:
Post a Comment