Katika ziara yao hiyo Dkt. Kikwete na mkewe
wamepata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ya mila na desturi za jamii hiyo
ya Wahadzabe hususan njia zao za asili za kutafuta na kuhifadhi vyakula, malezi
ya watoto, makazi yao, nk.
Pamoja na mambo mengine waliweza pia kuongea kwa
kina na wanajamii hao kuhusu changamoto zinazowakabili kama vile changamoto ya
upatikanaji wa elimu kutokana na mfumo wao wa maisha wa kuhamahama, uvamizi wa
makabila mengine katila maeneo yao ya asili hali inayotishia mtindo wao wa
maisha pamoja na upatikanaji wa huduma nyingine muhimu za kijamii.
Dkt. Kikwete alitumia fursa hiyo kuwapongeza
wenyeji wake kwa kuendelea kudumisha mila na desturi zao huku wakitambua na
kuzingatia umuhimu wa kuwapeleka watoto wao shule ili kupata elimu itakayokuja
kuwasaidia katika maisha yao ya baadaye.
Aidha, aliwataka viongozi wa Serikali
walioambatana naye kuzidisja ukaribu na jamii hiyo ili kusikiliza, kuzielewa na
kuzitafutia ufumbuzi changamoto za kipekee zinazoikabili jamii hiyo.
RAIS Mstaafu Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akiambatana na mke wake Mama Salma Kikwete wamezuru jamii ya
Wahadzabe wanaoishi katika Kijiji cha Endamagha kilichopo Kata Tarafa ya Eyasi,
Wilaya ya Karatu.








No comments:
Post a Comment