KAMATI YA MAANDALIZI WIKI YA REGROW YAKUTANA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, August 9, 2023

KAMATI YA MAANDALIZI WIKI YA REGROW YAKUTANA


NA SIXMUND BEGASHE

KAMATI ya Maandalizi ya maadhimisho ya wiki ya Mradi  wa Kuboresha Usimamizi wa Maliasili na Kukuza Utalii Kusini mwa Tanzania (REGROW), imekutana kwa kikao chake cha pili Mkoani Iringa ili kupata uwelewa wa pamoja na kuweka mikakati ya utekelezaji na ufanikishaji wa maadhimisho hayo.

 Akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya REGROW WEEK Bi. Hobokela Mwamjengwa ameeleza kuwa lengo la Wiki hiyo ni kuhabarisha wadau wa mradi na watanzania kwa ujumla kuhusu Mradi, fursa zilizoibuliwa, maeneo ya uwekezaji na wanufaika wa mradi kwa maslai mapana ya Taifa.

 

Naye Naibu Msimamizi wa Mradi wa REGROW Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Blanka Tengia, amefafanua kuwa mradi huo unaboresha miundombinu na kuzijengea uwezo wa kusimamia hifadhi za kipaumbele kwa lengo la kuziwezesha kutunza maliasili.

 Aidha Bi. Tengie ameongeza kuwa Mradi unaziwezesha jamii zinazoishi jirani na hifadhi za kipaumbele kukua kiuchumi pamoja na Kuboresha miundombinu ya umwagiliaji na usimamizi wa maji kwenye eneo la juu la Mto Ruaha Mkuu. 

 

Kamati hiyo  inajumuisha wajumbe kutoka TANAPA, Maafisa mbalimbali wa Serikali ya Mkoa wa Iringa, Jeshi la Polisi na Maafisa watekelezaji wa mradi wa REGROW Wizara ya Maliasili na Utalii, Bodi ya Utalii na Wakala wa Huduma za Misitu.

 

No comments:

Post a Comment