Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yatokanayo na Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Nane na wa Tisa wa Bunge iliyowasilishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma leo Agosti 09, 2023.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Dustan Shimbo akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo wakati wa kikao cha kikao cha kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yatokanayo na Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Nane na wa Tisa wa Bunge iliyowasilishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma leo Agosti 09, 2023.Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yatokanayo na Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Nane na wa Tisa wa Bunge iliyowasilishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma leo Agosti 09, 2023.
Makamu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo Mhe. Ramadhan Suleiman Ramadhan akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yatokanayo na Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Nane na wa Tisa wa Bunge iliyowasilishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma leo Agosti 09, 2023.(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
SERIKALI imesema
itaendelea kuhamasisha upandaji wa mikoko katika maeneo ya pwani kwa ajili ya
biashara ya kaboni na kusaidia kukabiliana na athari za mabadiliko ya
tabianchi.
Amesema hayo wakati
wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Utekelezaji
wa Maazimio ya Bunge yatokanayo na Uchambuzi
wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Nane na wa Tisa wa
Bunge iliyowasilishwa na
Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma leo Agosti 09, 2023.
Dkt. Jafo amesema
kuwa ni kweli maeneo ya pwani yanapata changamoto ya kuliwa na maji ya bahari
kutokana na kina kuongezeka hivyo Serikali inaendelea na jitihada za
kukabiliana na changamoto hiyo kwa kujenga kuta na matuta kwa ajili ya
kupunguza kasi ya mawimbi ya bahari.
Amesema katika
Biashara ya Kaboni Serikali inawakaribisha wawekezaji kutumia fursa hiyo kwa
kupanda mikoko katika maeneo hayo ya pwani yenye changamoto hizo za
kimazingira.
Amesema kuwa katika
baadhi ya maeneo ya pwani mikoko inachukuliwa na maji hivyo inasababisha kingo
za bahari kumomonyoka hivyo maji huingia nchi kavu na kusababisha mafuruko.
Aidha, Waziri Jafo
amewahimiza wakulima kuendelea kulima zao la korosho na kusema kuwa mbali ya
kuwapatia faida wakati wa uvunaji pia watafaidika na biashara ya kaboni hivyo
kuunga mkono juhudi za kupunguza hewa ya ukaa.
“Tutaendelea kutoa elimu kwa halmashauri nchini wapate utaratibu mzuri wa kuhusu kushiriki katika Biashara ya Kaboni kwani tayari tunashuhudia kule wilayani Tanganika wamenufaika,” amefafanua Dkt. Jafo.
(PICHA NA OFISI YA
MAKAMU WA RAIS)






No comments:
Post a Comment