TANZANIA inatarajia kuwa
mwenyeji wa Mkutano wa kimataifa wa chakula unaotarajiwa kufanyika Jijini Dar
es salaam kuanzia Agisti 10-12 Mwaka huu katika ukumbi wa Daimond Jublee
unaotarajiwa kuhudhuriwa na Makampuni zaidi ya 500 kutoka ndani na nje ya nchi
ya Wafanyabiashara, Wakulima na Wazalishaji .
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa
Pulses Ntwork (TPN) Zirack Andrew Jijini Dar es salaam amesema
katika siku hizo kutakuwa na mabanda ya maonyesho ya aina tofauti tofauti ya
mazao ya chakula kutoka katika kampuni mbalimbali hivyo kutakuwa
kongamono na midahalo mbalimbali na mainyesho na kunatarajia zaidi ya watu 3000
kutembelea mabanda kujifunza fursa zilizopo katika uzalishaji mazao ya chakula
kupitia teknolijia ya juu kutoka nchi za nje hivyo ni vyema wakulima kuhudhuria
ili kubadilishana uzoefu .
" Huu ni Mkutano unaofanyika kwa mara kwanza Afrika na mara ya kwanza Tanzania vyama tofauti tofauti vya vyakula Afrika tumeshirikiana kuwaleta wenzetu toka India. waliokuwa na uzoefu kufanya maonyesho kama haya miaka mingi sana India, Mashariki ya kati na sehemu nyingine tofaui tofauti Duniani ili kupata uzoefu na kuunganishwa na fursa ya kupata masoko ya kimataifa uuzaaji mazao ya chakula" amesema
Andrew amesema Dhima ya
Mkutano huu kimsingi ni kufungua masoko ya mazao Afrika nzima na duniani kote
kiujumla kwani miaka mingi iliyopita wakulima walikuwa wanalima mazao kwa ajili
ya kujikimu wao na familia zao siyo kuuza lakini miaka michache ya sasa
Wamehamia kutoka katika kilimo cha kujikimu na kulima kilimo cha kibiashara na
imekuwa na matokeo chanya kuongezeka sana kwa mazao ya chakula.
Naye Miongoni mwa Jopo la Waandaji wa Mkutano huo kutoka nchini
India Mkurugenzi wa Taso Event Suveer Rajapuexlint amebainisha kuwa nchi nyingi
za India, Asia, Mashariki ya kati na China zina idadi kubwa sana ya watu lakini
pia kipato chao cha mtu mmoja mmoja ni kikubwa sana akitolea mfano China ni
nchi ya pili kwa uchumi mkubwa pia India inaenda kwa kasi uchuminwake
hivi juzi juzi miezi miwili iliyopita India imeipita Uingereza kuwa ya ni nchi
ya 5 kwa uchumi mkubwa Duniani ina maana kuwa kipatao cha mtu mmoja mmoja
kimezidi kuongezeka hivyo nao wananunu chakula kutoka Tanzania.
"Mazao yakiwa mengi na
masoko hayapo inakuwa changamoto hivyo tumeangalia kuwa Kuna sehemu Duniani
wanakuwa na uhaba wa chakula lakini taarifa ya uzalishaji wapi watanunua chakula
hawana hivyo kupitia kongamano na mkutano huu sambamba na maonyesho
itasaidia wakulima kuunganishwa na wanunuzi wa mazao kutoka nchi ikiwemo
Asia, India, na china Mashariki ya kati "Suveer
Aidha watu wote wanakaribishwa kuweza kuhudhiria Mkutano huo kwani
kutakuwa na muda wa midahalo tofauti tofauti kutoka katika mazao ya aina
mbalimbali pia
wafanyabiashara watakutana
kuzungumza kwa pamoja na kuingia makubaliano ya kibishara ya siku chache za
usoni hivyo vikundi vya wakulima wafanyabiashara na watajionea fursa ya
teknolojia kutoka nje na kubadilishana uzoefu





No comments:
Post a Comment