Wakulima wadogo wa wakiangalia zao la Alizeti lililostawi katika udongo uliopimwa na kurutubishwa katika kijiji cha Izava.(Picha na Hamis Adam.)
TAASISI ya Utafiti wa Kilimo (TARI) Kituo cha Ilonga kinafanya utafiti wa zao la mikunde inayosaidia kurutubisha udongo kuwawezesha wakulima wadogo kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa na mazingira.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo
hicho, Dk. Emmanuel Chilagane amesema kuwa utafiti huo utawezesha wakulima
kutumia mbinu za kiasili na salama zaidi katika kurutubisha udongo.
Chilagane amesema kuwa kwa
sasa wanafanya utafiti katika mazao ya mikunde ikiwemo marejea, karanga,
maharagwe, kunde na njugu mawe ili kuweza kupata majawabu ya kutosha kuhusu
mazao hayo na kazi yake katika kurutubisha ardhi.
“Tunafanya utafiti kutokana
na mazingira mbalimbali na tabia za ardhi ya maeneo tofauti. Kiasili mazao hayo
yamekua yakitumika katika kurutubisha ardhi. Ila kutokana na mabadiliko ya
tabia nchi imetubidi kuangalia njia mbadala wa kurutubisha ardhi,” alisema.
Mtafiti na Mratibu wa
Kitaifa wa zao la Alizeti Frank Reuben amesema kuwa utafiti utazingatia
ushirikiano, mafunzo na ushamashishaji wa mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya
hali yahewa ili kujenga ustahimili wa mazao mbalimbali.
Reuben alisema kuwa utafiti
huo unawezeshwa na wadau mbali mbali toka sekta binafsi na taasisi za maendeleo
chini ya ungalizi wa Taasisi ya Uboreshaji wa Mifumo ya Masoko ya Kilimo (AMDT).






No comments:
Post a Comment