1. Mwenyekitiwa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe (kushoto),
akisisitiza jambo mbele ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi,
wakati wa kikao cha Msajili na viongozi waandamizi wa CHADEMA leo jijini Dar es
Salaam. Kikao cha Msajili na CHADEMA ni juhudi za ofisi hiyo kuimarisha hali ya
kisiasa hususan demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini.
1. Mwenyekitiwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe (kulia) akiteta jambo na Msajili wa Vyama vya Siasa,
Jaji Francis Mutungi (katikati), baada ya kumaliza kikao chenye lengo la
kuimarisha demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini kilichofanyika kwenye ofisi
ndogo za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar
es Salaam. Pembeni ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Myika.
NA MWANDISHI WETU
MSAJILI wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, leo jijini Dar es Salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa CHADEMA mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe yenye lengo la kuimarisha mazingira ya siasa hususani demokrasia ya vyama vingi vya siasa.
Viongozi wa CHADEMA walioambatana na Mbowe kwenye kikao hicho na Jaji Mutungi ni pamoja na Katibu Mkuu wa CHADEMA , John Mnyinka na Katibu wa Baraza la Wazee (BAZECHA), Rodrick Rutembeka.
No comments:
Post a Comment