Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na mwenyekiti wa Kituo cha
Demokrasia Tanzania (TCD) Profesa Ibrahim Lipumba Mkutano wa kitaifa wa wadau
kujadili hali ya demokrasia nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Vijiji,
Mitaa na Vitongoji mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu mwaka 2025 lililofanyika ukumbi
wa Diamond
DAR ES SALAAM
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kudumisha
demokrasia nchini kwa kuyafanyia kazi mapendekezo na michango mbalimbali
inayotolewa na vyama vya siasa, viongozi wa dini na asasi za kiraia kwa ustawi
wa demokrasia.
Mkutano huo umeandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kwa lengo la kujadili hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa maazimio ya Kongamano la kitaifa la Maridhiano, Haki na Amani na kuimarisha mapendekezo ya awali yaliyotolewa na wadau ili kuboresha mazingira ya kisiasa wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi mkuu 2025.
Vilevile, mkutano huo umehudhuriwa na Wawakilishi wa vyama vya siasa, viongozi kutoka Serikalini, Mabalozi na wadau wa demokrasia nchini.
No comments:
Post a Comment