NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Mohamed
Mchengerwa amsema tamasha la Kizimkazi ni miongoni mwa matamasha muhimu kwani
limeendelea kuwaunganisha wananchi wote bila kujali itikadi za siasa au dini.
Ametoa kauli hiyo kuelekea tamasha la Nane la Kizimkazi
baada ya kushuhudia mechi kati ya mashabiki wa Simba na Yanga wanaoishi
Makunduchi visiwani Zanzibar imedhaminiwa na Mwanamke Initiatives Foundation
chini ya Mwenyekiti wake Wanu Ameir Hafidh na imemalizila bila kupata mshindi,
hivyo itarudiwaAgosti 31,2023.
Akielezea zaidi kuhusu tamasha hilo ambalo linafadhiliwa na
kuratibiwa na Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation ambayo Mwenyekiti wake
ni Wanu Ameir Hafidh , Waziri Mchengerwa amesema tamasha hilo limekuwa
likiwakutanisha wananchi wa maeneo mbalimmbali nchini.
“Wanafika kwenye tamasha hilo bila kujali zao za vyama vya siasa
pamoja na itikadi za dini.Hiyo ndio inaleta tafsiri ya Tanzania na hiyo ndio
tafsiri ya Zanzibar.
“Kupitia matamasha kama haya watu wanakuwa wamoja, wanashikamana
pamoja bila kujali itikadi zao, kwa hiyo matamasha haya ni muhimu kwa vizazi
vya leo na kesho,”amesema Waziri Mchengerwa.
Kuhusu mechi ya mashabiki wa Simba na Yanga , amesema michezo
inatukumbusha kuwa na umoja, amani ndio kitu muhimu na wao ambao wako sekta ya
utalii wanaamini moja ya jukumu walilonalo ukiondoa vivutio vya asili
wanachojivunia nacho ni amani
“Utulivu ni kivutio kikubwa kwa nchi yetu , kwa taifa letu la
Tanzania ambalo linatofautiana na mataifa mengi duniani kwasababu amani
ukiitafuta utaipata Tanzania.”
CL - MICHUZI
No comments:
Post a Comment