TMA YATOA TAHADHARI, YATAJA MIKOA ITAKAYOKUMBWA NA UPEPO MKALI NA MAWIMBI MAKUBWA BAHARINI. - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, August 27, 2023

TMA YATOA TAHADHARI, YATAJA MIKOA ITAKAYOKUMBWA NA UPEPO MKALI NA MAWIMBI MAKUBWA BAHARINI.


MAMLAKA  ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyoitoa leo Agosti 27, 2023 imetoa tahadhari ya uwepo wa matarajio ya vipindi vya upepo mkali unaozidi km 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2.0 vinavyotarajiwa kutokea katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya Kusini ya Bahari ya Hindi ikihusisha mikoa ya Lindi na Mtwara pamoja na Ukanda wa Ziwa Victoria ikihusisha mikoa ya Kagera ,Mwanza, Mara, Geita na Simuyu kwa Ziwa Nyasa mikoa husika ni Ruvuma, Njombe na Mbeya alikadharika kwa eneo la Ziwa Tanganyika itahusisha mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa.

Taarifa hiyo ya TMA, pia imetoa angalizo kuwepo kwa upepo mkali unaofikia km 40  kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita 2.0 yanayotarajiwa kutokea kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa Pwani ya Kaskazini ya Bahari ya Hindi inayojumuisha visiwa vya Mafia, Ungunja na Pemba pamoja na mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Pwani, huku wananchi wakitahadharishwa kuwa makini makini na hali hiyo.

No comments:

Post a Comment