WAGOMBEA UDIWANI 136 WA CCM MKOANI PWANI WATAJWA UCHAGUZI MKUU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, August 16, 2025

WAGOMBEA UDIWANI 136 WA CCM MKOANI PWANI WATAJWA UCHAGUZI MKUU

 


NA MWANDISHI WETU, KIBAHA

WAGOMBEA Udiwani 136 ambao wameshinda kura za maoni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani wamepitishwa kuwania nafasi hiyo kwenye uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Mjini Kibaha Katibu wa Siasa Uenezi na Mafunzo Mkoa wa Pwani David Mramba alisema kuwa madiwani hao ni wale walioongoza kwenye kura za maoni.


Mramba alisema kuwa madiwani hao ni wale walioshinda kwenye Kata 136 hivyo kupata fursa kuingia kwenye kinyanganyiro na wagombea wa vyama vingine.


Alisema kuwa walioshinda siyo kwamba ni bora sana bali nafasi ilikuwa ni moja tu hivyo wawakilishe vyema chama kwenye uchaguzi mkuu.

Mkoa una jumla ya Kata 136 hivyo kufanya madiwani 183, Viti MaalumTarafa ni madiwani 27, na wagombea kupitia kapu ni wawili hivyo kufanya jumla 185.


Aidha alisema kuwa majina hayo yamerudishwa kutoka CCM Makao Makuu baada ya uchaguzi wa kura za maoni zilizofanyika kote nchini.

No comments:

Post a Comment