MAGIC VIBE AWARD KUFANYIKA MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM NOVEMBA 19 MWAKA HUU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, October 9, 2023

MAGIC VIBE AWARD KUFANYIKA MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM NOVEMBA 19 MWAKA HUU




NA MAGENDELA HAMISI

TUZO inayofahamika kwa jina la Magic Vibe kwa mwaka huu zinatarajiwa kufanyika Tanzania kwa mara kwanza katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam Novemba 19 mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Oktoba 9, 2023, Mratibu wa tuzo hizo hapa nchini Seif Khalid, amesema kwamba Magic Vibe Award kwa mara ya kwanza mwaka jana (2022) zilifanyika Texas nchini Marekani. 2022.

Amesema kutokana na changamoto kadhaa zilizojitokeza mwaka jana nchini humo, ikiwemo baadhi ya wasanii wa Afrika Mashariki kushindwa kuudhuria licha ya kukatiwa tiketi ya ndege, ndiyo sababu iliyofanya mwaka huu hapa Tanzania kwa mwaka huu.

“Tumeamua tuzo hizi kuzifanya hapa Tanzania kwa mwaka huu kutokana na baadhi ya wasanii, waliotakiwa kwenda kwenye tuzo hizo nchini Marekani ni mwaka jana kushindwa kufanya hivyo licha ya kukatiwa tiketi ya ndege.

Sababu nyingine ya kuleta tuzo hizi hapa nchini kwa mwaka huu ni kutokana na Tanzania kuwa kitivo cha burudani na itasaidia kuleta hamasa kwa wasanii kujiweka sawa kufanyua kazi nzuri zitakazoleta ushindani kwa wasanii wa Afrika Mashariki," amesema.

Ameongeza kuwa siku hiyo ya tuzo wasanii mbalimbali wa Afrika Mashariki wataudhulia jambo litakalofanya kuwepo kwa shoo kabambe na mwakani pia inatarajiwa kufanyika tena hapa nchini na tarehe ikiwa tayari imepangwa kufanyka Oktoba,4 2024.

Aidha ameongeza kuwa baada ya tuzo hizo za mwakani, mwaka 2025 zitafanyika nchini Kenya na mwaka 2026 zitafanyika na mwaka 2026 zitafanyika Uganda na baada ya hapo zitarejeshwa kufanyika nchini Marekani.

Amefafanua kuwa kwa mwaka jana ambapo ziliafanyika kwa mara ya kwanza nchini Marekani zilikuwa katika kategori 20 na mwaka huu zimeongezwa kategori saba hivyo zitakuwa 27 hali ambayo inatoa fursa kwa

wasanii, madj na kufanya vema na kujiwerka katika mazingira mazuri ya kujitangaza kimataifa kupitia kazi zao.

"Ninachoomba ni kwa wasanii ambao wamo katika kuwa kuwania Magic Vibe Award kuwaomba mashabiki wao kuwapiga kura kuanzia sasa hadi Oktoba 31, 2023 kupitia website www.magicvibeawards2023.com na tiketi

za kuingia katika tuzo hizo zinauzwa katika vituo vya Mac Juice - Sinza, Vunja Bei- Sinza, Sharobaro wa Instagram- Sinza Mori na Magomeni Kanisani na kwa Mr Chambuu Sinza Makuburini," amesema

Khalid ameongeza kuwa vigezo vya wasanii kushiriki katika tuzo ni pamoja na kufaya vizuri katika kazi zake na namna anavyoutambulisha kimataifa na kingine ni namna anavyoweza kuwa imara kimuziki kwa kipindi kirefu bila kushuka.

Burton Mwambe maarufu kwa jina la Mwijaku ambaye alikuwa sehemu ya wazungumzaji kuelekea siku ya tuzo hizo, amesema kuwa tuzo hizo zitaleta ushindani kwa wasanii mbalimbali jambo litakalosaidia kuendelea

kuukuza muziki wa Tanzania ndani na nje ya nchi.

"Tunakwenda kuleta mageuzi ya kimuziki kupitia tuzo hizi ambazo zinafanyika nchini kwa mara ya kwanza na mara pili baada ya kufanyika mwaka jana nchini Marekani, hivyo nawaomba wasanii watakaingia kuwania waache kasumba ya kukacha kama inavyotokea katika tuzo nyingine.

"Hiki ni kipimo chao cha kweli katika kufanya vizuri kimuziki na si kule kwenye twiter,tik tok, Istagram na kwingineko kwenye mitandao ya kijamii ambapo wanaonekana kufanya vizuri ila naamini walishiriki kwenye Magic Vibe Awards kwao ndicho kitakuwa kipimo halisi cha kufanikiwa ndani na kimataifa, amesema.

Pia Mwijaku aliomba taasisi, mashirika na kampuni mbalimbali kujitokeza kudhamini tuzo hizo ili kufanikisha vijana kupata mafanikio na kupiga hatua kimuziki kupitia shindano za kuwania tuzo hizo na

ikizingatiwa kuwa wiki hii ni wiki wa vijana hivyo ni vema wakaungwa mkono na taasisi hizo.


No comments:

Post a Comment