BRELA YAIKABIDHI CHANETA VIFAA YA MICHEZO - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, November 22, 2023

BRELA YAIKABIDHI CHANETA VIFAA YA MICHEZO

NA MWANDISHI WETU

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imekabidhi  vifaa vya michezo 'truck suits' jozi 25 pamoja na mipira mitano kwa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) vitakavyotumiwa na timu ya Netiboli Wanawake,( Taifa Queens).

Akikabidhi  vifaa hivyo leo Novemba 22, 2023, Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA , Loy  Mhando amesema  BRELA  ni mdau mkubwa wa michezo,  kwakuwa inatambua kuwa michezo  ni afya, ni burudani pia kupitia michezo taasisi inajitangaza na zaidi ya hapo michezo  ni biashara hivyo kama taasisi inayohusika na masuala ya urasimishaji biashara ina wajibu wa kushirikiana na wana michezo nchini.

 "BRELA imekuwa ikishiriki katika michezo mbalimbali na kutoa misaada kwa wadau wa michezo ili kuhakikisha kuwa sekta ya michezo nchini inakuwa na kujipambanua kimataifa", amefafanua, Mhando.

Aidha, Mhando  amesema msaada wa vifaa uliotolewa  unaunga  mkono jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha ukuaji wa sekta ya michezo  nchini.   

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa  CHANETA, Rose Mkisi ameishukuru BRELA kwa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu ya Taifa Queens .

“Tunaishukuru sana BRELA kwa msaada wa vifaa vya michezo na tunaahidi kupitia vifaa hivi vya michezo timu ya netiboli itafuzu vyema  katika michuano mbalimbali watakayoshiriki. 

BRELA  imetoa msaada wa vifaa hivyo baada ya kupokea maombi kutoka CHANETA kuhusu uhitaji wa vifaa vya michezo  vitakavyotumika  katika mashindano mpira wa pete  nchini Botswana.

Hafla hiyo ya makabidhiano ya vifaa vya michezo  imefanyika katika Ofisi za BRELA jijini Dar es Salaam.




No comments:

Post a Comment