NA MAGENDELA HAMISI
NAIBU Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 16 ya Chuo cha Kodi (ITA), yatakayofanyika Novemba 24, 2023 katika ukumbi wa chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Isaya Jairo “ Naibu Waziri wa Fedha, atakuwa na jukumu la kuwatunuku vyeti wahitimu wa ngazi Shahada na Stashada na waliofanya vema katika masomo yao.
Ameongeza kuwa mahafali hayo yanafanyika huku chuo hicho kikiwa kinajivunia mafanikio kadhaa katika kutekeleza mpango mkuu wa tano ambao umejikita kutoa mafunzo kwa nmjia ya kisasa ya kigitali.
Amefafanua kuwa chuo hicho ni hapa nchini na Afrika Mashariki na Kusini chenye usajili na Ithibati ya kudumu ya kutoa mafunzo ya Forodha na Kodi kwa wadau mbalimbali katika ngazi ya astashahada, shahada na shahada ya uzamivu.
Aidha amefafanua kuwa chuo hicho kinachotoa mafunzo yanayoendana na mabadiliko ya sayanasi na tenknolojia na uchumi yanayolenga mahitaji ya soko la wataalamu wanaohitajika katika nyanja ya forodha na kodi nchini na duniani kwa ujumla.
Tofauti na hayo Mkuu huyo wa Chuo, amesema kuwa pia wanatoa ushauri na kuwajengea uwezo watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Mapato Zanzibar na Mamlaka nyingine Afrika.
“Jumla ya wahitimu 508 wanatarajiwa kutunukiwa vyeti kati yao 293 ni wanaume na 215 ni wanawake ambapo watakaotunukiwa cheti cha Uwakala wa Forodha Afrika Mashariki watakuwa 253, wahitimu wa 52 watatunikiwa cheti cha Stashaha ya Uzamili ya chuo cha kodi.
Pia wahitimu 43 watatumikiwa cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi, 39 watatunikiwa cheti cha Astashahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi, wahitimu nne watatunukiwa cheti cha Astashahada ya Juu ya Forodha na Kodi na 117 watatunukiwa Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi
Ameongeza kuwa katika mahafali hayo ya 2022/23 wameharika baadhi ya Mamlaka za Usimamizi wa kodi kutoka Afrika, Uganda ndio kwa sasa wamethibitisha kushiriki katika shughuli hiyo.





No comments:
Post a Comment