JESHI LA POLISI LIMEPOKEA MAGARI 43 KUTOKA KAMPUNI YA ASHOK LEYLAND - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, November 21, 2023

JESHI LA POLISI LIMEPOKEA MAGARI 43 KUTOKA KAMPUNI YA ASHOK LEYLAND

                                                          ....................................................

NA MWANDISHI WETU

JESHI  la Polisi, limepokea magari 43 kutoka Kampuni ya Ashok Leyland ikiwa ni jitihada za Serikali kuliwezeshwa jeshi hilo kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Akiongea katika hafla ambayo imeanyika leo Novemba 21, 2023 katika Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Jumanne Sagini, amesema magari hayo yametokana na mkataba wa masharti nafuu wa mwaka 2013 kati ya Serikali ya Tanzania na India ambapo ulikuwa na jumla ya magari 881 na baadhi ya magari mengine yalishawasili nchini na kusalia magari 200.

 “Tupo katika hatua za mwisho kupokea magari yaliyosalia ambapo leo tumepokea magari 43," amesema Sagini.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri,Sagini amelitaka Jeshi la Polisi kutenga bajeti za matengenezo ya mara kwa mara ya magari hayo ili yaweze kudumu kwa muda mrefu.Pia amewataka  wawakilishi wa Kampuni ya Ashok Leyland na mdau wake Kifaru Motors kuhakikisha upatikanaji wa msaada wa kiufundi na vipuri pale itakapohitajika.

Akiongea kwa niaba ya  Mkuu Jeshi la Polisi Nchi, Kamishna wa Polisi Menejimenti ya Rasilimali watu, CP. Suzan Kaganda amesema magari hayo yatatumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuliwezesha Jeshi la Polisi katika maboresho yanayoendelea ili kuongeza ufanisi wa kutoa huduma kwa wakati  kwa wananchi.

Kwa upande wake Naibu Balozi wa India hapa nchini, Manoj Varma amesema  ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na India ni wa muda mrefu ambapo makabidhiano ya magari kutoka Kampuni ya Ashok Leyland italisaidia Jeshi la Polisi kutimiza majukumu yake kwa urahisi na kwa wakati.




.......................................................................................



No comments:

Post a Comment