Mkurugenzi Mkuu wa LHRC, Dk. Anna Henga
...................................................................................
NA SELEMANI MSUYA
IKIWA
zimepitasiku 11 baada ya Serikali kuwasilisha miswaada mitatu bungeni, Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimeanisha upungufu wa miswada hiyo na kutoa
mapendekezo, huku ikisisitiza muarobaini ni kupatikana kwa KatibaMpya.
Miswada
hiyo ni pamoja na Muswada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Muswada wa Sheria
ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama
vya Siasa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi, yote ikiwa ya mwaka 2023.
Upungufu
wa mapendekezo kuhusu miswaada hiyo yametolewana Mkurugenzi Mkuu wa LHRC, Dk.
Anna Henga wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Dk.
Henga amesema LHRC inapongeza Serikali kuwasilisha miswaada hiyo bungeni na kuwa
hiyo ni dalili ya usikuvu kwa viongozi na kuwataka wananchi kujitokeza kuto amaoni.
Amesema
miaka zaidi ya thelathini (30) tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, mwaka
huu Serikali imeridhia madai ya muda mrefu kutoka kwa wadau wa demokrasia ya vyama
vingi nchini kwa kuwasilisha miswada hiyo muhimu kwa taifa.
Mkurugenzi
huyo amesema katika miswada hiyo kuna baadhi ya mambo ambayo ni ya kupongezwa. kwa
mfano suala la mgombea kupita bila kupingwa, kuanzishwa kwa Kamati ya Usaili kwa
wajumbe watume ya uchaguzi na maamuzi ya Ofisa Mwandikishaji kupingwa mahakamani.
“Hata hivyo miswada hiyo ina upungufu ikiwemo Mkurugenzi wa Uchaguzi kuwa Katibu wa Kamati ya Usaili.Sheria imeanzisha kamati ya usaili ambayo kazi yake ni kusaili wajumbe wa Tume yaUchaguzi.
Kwa
mujibu wa kifungu cha 9(3) cha muswada, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
atakuwa katibu wa kamati ya usaili inayoanzishwa chini ya kifungu cha 9(1) cha
muswaada, kitendo kinachoashiria mkanganyiko wa wazi. Kwa mujibu wakifungu cha
18 cha muswada, kwa kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi
atapatikana kwa kuteuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na tume,” amesema.
Dk
Henga amesema swali la msingi linakuwa kipi kinaanza katika ya tume na mkurugenzi
wa uchaguzi? Wakati mkurugenzi anakuwa katibu wa kamati ya usaili, kamati yenye
jukumu la kutafuta wajumbe wa tume maana yake kwa wakati huo tume inakuwa bado haijapatikana.
Henga
amesema kwa mazingira hayo mkurugenzi hawezi kuwa katibu wa kamati ya usaili wakati
anapatikana kwa kuteuliwa na Rais baada ya kupendekezwa na tume.
Mkurugenzi
huyo amesema LHRC inapendekeza marekebisho ya kifungu hicho na kutafuta mtu mwingine
atakayekuwa katibu wa kamati ya usaili kwa hoja kuwa wakati huo hakuna tume,
hivyo wanashauri mwenyekiti wa bodi ndio awe Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
ili bodi iwe na mamlaka ya kusimamia mchakato mzima wa kuajiri watumishi wa tume.
Mkurugenzi
huyo amesema eneo lingine ambalo wanaona lina upungufu kuhusu watumishi wa umma
kuendelea kuwa sehemu ya tume, jambo ambalo linakiuka amri ya Mahakama ya Rufaa
na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ambayo imetoa maamuzi kuwa sio
halali watendaji hao kusimamia uchaguzi.
“Moja
ya malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wadau wa demokrasia nchini ni tume kutumia
watumishiwa umma katika michakato ya kiuchaguzi. Kwa mujibu wa kifungu cha 21
cha muswada, tume itaendelea kutumia au kuazima watumishi wa umma kuwa wasimamizi
wa uchaguzi, kwa lugha nyingine wakurugenzi na watumishi, hii sio sawa, hata mahakama
imekataa,” amesema
Amesema
lugha iliyotumika ni kuazima, lakini ukweli ni kwamba watumishi wa umma wataendelea
kuwa sehemu ya tume kinyume na matarajio ya wadau walio wengi.
Dk
Henga amesema LHRC inapendekeza tume ipewe uwezo wa kuajiri watumishi wake
wenyewe kuanzia ngazi ya kata, wilaya, mkoa na Taifa badala ya kuendelea kuazima
watumishi wa umma.
Mkurugenzi
huyo amesema pia wanashauri tume iwe inapata fedha kutoka hazina moja kwa moja na
sio kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, kwani kitendo hicho kina inyima uhuru.
Aidha,
amesema tume kushauriana na waziri mwenye dhamana na masuala ya utumishi kuandaa
muundo wa utumishi wa Sekretariati ya Tume, kwa mujibu wa kifungu cha 23 cha muswada,
hiyo inaashiria tume itaendelea kupokea maelekezo kwenye mamlaka nyingine za Serikali.
Akizungumzia
kifungu cha 18 cha muswada kutaka mkurugenzi wa tume kuwa ofisa mwandamizi wa umma,
hakina mashiko na kwamba ni vema ziwepo sifa nyingine zaidi zinazoruhusu watu kutoka
maeneo mengine.
Dk
Henga amesema hoja ya mpiga kura aliyepoteza kitambulisho au kufutika kutakiwa kulipa
fedha ili apate upya haina mashiko na kwamba inakiuka Katiba ya Tanzania ya mwaka
1977 kwa mujibu wa ibara ya 5 na 21.
“Moja
ya mambo ya kutia moyo katika muswada huu ni pamoja na uwepo wa takwa la
mgombea kupita bila kupingwa katika nafasi zote za Rais, Ubunge na Udiwani, na Ofisa
Mwandikishaji kupingwa Mahakamaya Wilaya,” amesema.
Kwa
upande mwingine Dk Henga amesisitiza kuwa ili Tanzania kuondoka kwenye mkwamo wa
kisheria na malalamiko ya wadau wa siasa, muarobani ni kutengeneza Katiba Mpya ambayo
itagusa sekta zote.





No comments:
Post a Comment