NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO AZINDUA MNADA WA KWANZA TANZANIA WA CHAI MTANDAONI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, November 13, 2023

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO AZINDUA MNADA WA KWANZA TANZANIA WA CHAI MTANDAONI

 

   Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Dkt. Hussein Omari akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo, Novemba 13 jijini Dar es Salaam.                                

NA MAGENDELA HAMISI

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Dkt. Hussein Omari, akimwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo. Hashim Abdallah amewataka wamiliki wa viwanda vya chai ambavyo havifanyikazi kuvifufua na kuhimalisha mitambo yao.

Pia ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda kufanya kila liwezekanalo kufanikisha malipo kwa kwa wakulima na wazalishaji wa zao hilo ili kusaidia kuongeza chachu ya uzalishaji itakayoendana na mahitaji ya soko.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua Mnada wa Chai,Tanzania kupitia mtandao ambao wanunuzi duniani kote watakuwa na fursa ya kununua zao jambo litakalosaidia taifa kunufaika kupitia kutanua wigo kibiashara.

“Kutokana na mchakato huu kukamilika niwaahidi Serikali inaweka mazingira wezeshi ili kufanikisha uwekezaji wenye tija katika sekta ya kilimo cha chai nchini na mnada utakuwa uendelevu na ninaomba taasisi zinazosimamia zao zihakikisha ubora wa chai unahimarika ili isaidie kila mkulima wauze angalau asilimia 15 katika mnada,” amesema.

Ameongeza kuwa hadi kufanikiwa kuanzishwa kwa mnada huo ni juhudi kubwa imefanyika kupitia Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kuingiza fedha nyingi kwenye maendeleo ya kilimo nchini.

Pia ameipongeza Bodi ya Chai Tanzania kwa hatua hiyo kwa maana ni hatua kubwa katika kuleta mendeleo ya kilimo na ukuaji wa zao la chai nchini na kuweka wazi kuwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo inatambua kazi kubwa iliyofanywa na bodi hiyo na wadau wengine ikiwemo sekta binafsi.

“Niwasisitize wakulima na wazalishaji wa chai nchini kuhakikisha mnapamana vya kutosha ili kuhimili ushindani kwa kuzalisha chai iliyo bora jambo litakalosaidia kupata mafanikio kupitia mnada huu wa kimtandao kwa kupata masoko mengi zaidi duniani,”amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania Mary Kipeja amesema kwamba pamoja na kuchelewa kuanza kwa mnada huo lakini anaamini itakwenda vizuri kwani wameanza vizuri tangu Julai mwaka huu.

“Mnada huu utakuwa na manufaa mengi sana, hii itawashawishi hata wasindikaji wa chai kuja nchini kwa wingi kwani gharama zitapungua na faida ya zao la chai itaongezeka. Hata mkulima mdogo atapata faida,” amesema Kipeja.

Kipeja ametaja baadhi ya changamoto zinazoukabili mnada huo kuwa ni pamoja na ufinyu wa bajeti wa kuutangaza hadi nje ya nchi, ufinyu wa bajeti ya kusajili na kuwapatia wakulima vyeti vya ubora ili Kufikia viwango vya kimataifa.

Nyingine ni ufinyu wa bajeti ya kutumika katika kushawishia nchi za jirani kutumia mnada wa Tanzania kuuza chai yao na kutokana na changamoto hizo aliiomba Wizara ya Kilimo kusadia bajeti ya kutosha ili kufikia malengo ambao wamejiwekea.






 

No comments:

Post a Comment