TIMU ya Tanzania ya kuogelea ambayo imeshiriki mashindano nane Kanda ya tatu , 2023 imefanikiwa kurejea salama nyumbani ikiwa imeshika nafasi ya pili ya ushindi wa jumla kati ya mataifa 10 yaliyoshiriki michuano hiyo Kigari nchini Rwanda.
Mashindani hayo yaliyokuwa yakichezwa kwenye viwanja vya michezo Ghanga Club House La Pallisse Arena katika Jiji la Kigari, nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Uganda, ya tatu ilichukuliwa na Kenya ya nne ilichukuliwa na wenyeji Rwanda ya tano ilichukuliwa na Burundi.
Nafasi ya sita ilichukuliwa na Afrika Kusini ya saba ilitwaliwa na Eswatini, nane ni Eritrea, tisa ni Djibouti na iliyofunga dimba ni Ethiopia.
Kocha wa timu hiyo, Alexander Mwaipasi ameongeza kuwa tofauti na kushika nafasi ya pili pia wachezaji wake wameshinda vikombe kadhaa kwenye nafasi walizoshindana na kuwataka ambao wametwaa medali ni Collins Saliboko (17) amepata medali ya dhahabu.
Mwingine ni Aryan Bhattbhatt ambaye alishindana kwa umri wa miaka 15-16 amefanikiwa kupata medali ya dhahabu katika michezo yake yote saba aliyoshindana, Max Missokia akishndana katika umri wa miaka 11-12 kwa upand wa wavulana amefanikiwa kupata medali za dhahabu kwenye michezo yake aliyoshiriki.
Mwingine ni Romeo Mwaipasi ambaye wa ameshika nafasi ya pili kwa mashindano ya miaka 15-16 kwa wavulana na akafanikiwa kupata medali ya dhahabu baada ya kufanya vizuri katika michezo yake.
Pia Austin Okore amepata medali ya dhahabu kwa mashindano ya umri wa miaka 13-14 baada ya kufanya vizuri katika michezo ambayo amecheza na Filbertha Demello amefanikiwa kuwa wa kwanza kwa umri wa miaka 13-14 kwa wasichana na kutwaa medali za dhahabu katika michezo yake yote aliyoshiriki
Crissa Dillip amekua wa pili kwa mashindano ya umri wa miaka 13-14 wasichana na kupata medali za dhahabu katika michezo yake yote aliyoshiriki naye Muskan Gaikwad amekuwa wa tatu kwa wasichana wa umri wa miaka 17 na kutwaa medali za dhahabu katika michezo yake yote aliyoshiriki.
Ameongeza kuwa anapenda kuwatambua wachezaji ambao mchango umefanikisha timu kushika nafasi ya pili wa jumla ikiwa ni kwenye mbio zao binafsi au mbio za kupokezana na kufanikiwa kupata jumla medali 127 na vikombe vinane.






No comments:
Post a Comment