“TUNAENDA KUYAFANYIA KAZI MAPENDEKEZO YA TENMET: DKT RWEZIMULA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, November 29, 2023

“TUNAENDA KUYAFANYIA KAZI MAPENDEKEZO YA TENMET: DKT RWEZIMULA

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dkt. Franklin Rwezimula akizungimza na wanahabari baada ya kufunga kongamano la elimu lililoandaliwa na TENMET.

                                               ..............................................................................

NA MAGENDELA HAMISI

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dkt. Franklin Rwezimula amesema kuwa Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) unaisaidia Serikali katika kupanga mipango yake katika sekta ya elimu nchini hususan maeneo ya kundaa sera na miongozo inayoaendana na wakati.

Pia amefafanua kuwa wamekuwa wakipata mawazo mengo katika kuandaa miundo mbinu ya elimu, mitaa pamoja na kuwapata walimu bora wanaweza kuwaanda vema wanafunzi  jambo ambalo linalisaidia taifa kupata mafanikio kupitia nyanja hiyo.

“Tunaenda kuyafanyia kazi mawazo yaliyotolewa na TENMET ambao ni wadau wa kubwa wa Serikali katika nyanja ya elimu na tunaamini matokeo yatakuwa mazuri ambayo yatalisaidia taifa kuondoa changamoto mbambali  na kuboresha mazingira ya elimu nchini ili kumkomboa mtoto wa kitanzania,” amesema.

Dkt Rwezaula akifunga kongamono la siku tatu leo Nov 29, 2023 jijini Dra es salaam lililoandaliwa na  TENMET, amefafanua kuwa ni jambo jema kuona mashirika na taasisi zikiandaa makongamano ya elimu kwa lengop la kuisaidia Serikali kufanya vema katika nyanja hiyo na wataendelea kutoa ushirikiano kwa wadau  hao wa elimu nchini.

Faraja Nyarandu ambaye ni Mwenyekiti wa TENMET, amesema ni jambo zuri kuona Serikali ikiunga mkono juhudi zao katika kuhakikisha Tanzania inapiga hatua kubwa katika nyanja ya elimu ambayo ndio mkombozi wa kijana wa kitanzania.

Aliongeza kuwa kwa sasa elimu imekuwa na ushindani mkubwa katika soko kulingana mahitaji ya dunia hivyo kama kijana anapata elimu ya kawaida ni dhahiri anaweza kukwama katika michakato yake ya kujitafutia maisha hivyo ni vema kutafuta mbinu zitakazosaidia kuboresha elimu ili kuendana na mahitaji ya sasa.

"Hivyo tunashukuru kuona Serikali ikichukua maoni yetu na kwenda kuyafanyia kazi, tunaamini mambo yatakuwa mazuri siku za usoni na elimu yetu itakuwa bora zaidi kulingana na mahitaji na mabadiliko kadhaa ya sayansi na teknolojia" amesema.

 

No comments:

Post a Comment