TBA YAANZA KUWAONDOA WADAIWA SUGU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, November 29, 2023

TBA YAANZA KUWAONDOA WADAIWA SUGU

*  WATOTO WACHUKULIWA SHULE JUU KWA JUU WASISHUHUDIE TUKIO HILO 

 NA MAGENDELA HAMISI

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) wameanza kuwandoa wapangaji wake ambao ni wadaiwa sugu wakiwa wameishi katika nyumba hizo na kushindwa kulipa kodi zao kwa wakati na kusababisha malimbikizo kufikia Shilingi bilioni 1.1.

Akuzungumza leo katika mchakato wa kuwaondoa wapangaji katika nyumba zao za Mbezi Beach jijni Dar es Salaam Kaimu Meneja wa TBA, mkoani Dar es Salaam Arch. Bernald Mayemba amesema kuwa zoezi hilo halitamuonea mtu yeyote na wala hawataangalia cheo cha mtu.

“Kimsingi mchakato wa kuwaondoa wapangaji ambao ni wadaiwa sugu kwa Mkoa wa Dar es Salaam lilitakiwa kuanza Desemba Mosi mwaka huu ila kutokana na dalali wetu wa makahama kukamilisha zoezi la notisi kwa siku 10 nyuma hatukuona sababu za kusubiri Desemba Mosi.

“Limeanza leo hapa Mbezi Beach na baada ya hapa tutaenda katika maeneo mengine ikiwamo Masaki, Mikocheni, Chang’ombe, Chole Onela Temeke na maoneo myote ya Dar es Salaam na hakuna atakayeachwa katika zoezi hili,” amesema.

Ameongeza kuwa mchakato wa kuwaondoa wadaiwa sugu litandelea kwa wiki tatu kuanzia jana, hivyo ametoa wito kwa wadaiwa wote ambao bado hawajafikiwa na zoezi hilo kulipa madeni yao haraka kwa maana mdaiwa yeyote atakayelipa saa mbili kabla ya zoezi hilo ataondolewa na hatoachwa.

Alifafanua kuwa kila mdaiwa lazima deni hilo licha ya kuondolewa katika nyumba hizo na taratibu za kisheria zitatumika kuhakikisha madeni yote yanalipwa.

Ameweka wazi kuwa ili kuepusha kadhia hiyo ya kuwaondiosha wadaiwa sugu, tayari mchakato wa mpangaji kulipa deni pango la nyumba kupitia makato katika mshahara wake na pindi utakapokamilika utaanza kutumia rasmi.

Wakati mchakato wa kuwaondoa wadaiwa hao sugu ukiendelea, mmoja wa mashuhuda aliuambia MAGENDELA BLOG kwamba baadhi yao wamekwenda kwenye shule wanazosoma watoto wao na kuwandosha kuwapeleka kwa ndugu zao ili wasione tukio hilo.

Unajua ndugu wakati mnakuja tu hapa mmoja wa wapangaji ambaye anaondoshwa kwenye hizi nyumba ametuma mfanyakazi wake wa ndani aende shule haraka wanaposoma vijana wake awachukue na awapaleke kwa ndugu zao ili waisone aibu hii ambayo inaweza kuwaathiri kimasomo na kwenye ukauaji wao.

 




 

 

 

No comments:

Post a Comment