UJENZI WA BWAWA LA TLAWI WAFIKIA 95%, NDOTO YA WAKAZI WA TLAWI YATIMIA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, November 12, 2023

UJENZI WA BWAWA LA TLAWI WAFIKIA 95%, NDOTO YA WAKAZI WA TLAWI YATIMIA


****************************************************

NIRC, MANYARA 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa mradi Bwawa la Tlawi, unaojengwa katika kijiji cha Tlawi, Kata ya Tlawi,Tarafa ya Endagikoti, Halmashauri ya Mji wa Mbulu mkoani Manyara,unaogharimu bilion 6.4,utakaonufaisha wakulima wa zao la vitunguu swaumu pamoja na mazao mengine.

Akizungumza katika ziara ya kamati hiyo Mwenyekiti wa Kamati, Daniel Sillo, amesema kukamilika kwa mradi huo ,kutaongeza pato la  mtu mmoja mmoja na  taifa kwa ujumla, hivyo mradi huo pamoja na miradi mingine, itachangia ongezeko la fedha katika bajeti ya Serikali.

Aidha, Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde, amempongeza Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa ,kwa usimamizi thabiti wa miradi ya ujenzi, miundombinu ya umwagiliaji.

Sanjari na hayo, Silinde amewaasa wakulima wa eneo hilo kuutunza na kuulinda mradi huo, ili uwe na tija, katika kukuza sekta ya umwagiliaji nchini.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mndolwa amesema, Tume itahakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa, ambapo hadi sasa mradi umefikia 95%,ambapo jumla wakulima 2400 watanufaika.

Mndolwa ameongeza kuwa, miradi yote inayojengwa itakamilika kwa wakati, na Serikali inaendelea kutoa fedha kwa aajili ya utekelezaji.

Mradi wa ujenzi bwawa la umwagiliaji Tlawi, baada ya kukamilika,utaongeza eneo la umwagiliaji  kutoka Hekta 5 mpaka zaidi ya Hekta 90,na wakulima wataweza kulima msimu mmoja hadi mitatu kwa mwaka,pamoja na kuzalisha ajira kwa jamii inayozunguka mradi huo.





No comments:

Post a Comment