MAGENDELA HAMISI
SERIKALI ya Awamu ya Sita chini Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, inaendelea na mchakato wa ujenzi wa vyuo vingine vitatu vya ufundi stadi kwa lengo la kuhakikisha vijana wanapata fursa ya masomo na kuwa na ujuzi na maarifa utakawasaidia kujiari na kuwaajili wengine na kuondokana na changamoto ya ajira nchini.
Vyuo hivyo vitatu vinaendelea kujengwa katika Wilaya za Ubungo,Kinondoni na Kigambani na vikikamilika moja kwa moja vitakuwa chini ya usiamamizi wa VETA na itafanya Kanda ya Dar es Salam kuwa na vyuo vitano.
Hayo yamebainishwa Desemba 19 na Mkurugenzi wa Vyuo vya Veta Kanda ya Dar es Salaam, Angelius Ngonyani wakati wa mahafali ya 12 ya Chuo cha Veta Kipawa jijini Dar es Salaam ambacho kipo kimkakati kwa ajili ya kutoa mafunzo ya Habari na Mawasiliano TEHAMA.
“Chuo hiki cha Kipawa ni chuo cha kimakakati kwa maana kimejikita katika kutoa mafunzo upande wa teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na program zote zinalenga katika maeneo hayo na kuna mpya unatolewa unaoitwa Mikertronic ambao ndio uofanyakazi zaidi kutokana na mabadiliko ya viwanda na viwanda vingi ndio vinahamia katika utendaji kazi katika upande huo na kuachana na alogi,” amesema.
Ameongeza kuwa kati ya wahitimu 314 wa fani ya ICT, udereva na Umeme katika nzadi ya daraja la pili na tatu, 32 pekee ndio wamekuwa wakichukua kozi mpya ya Mikertonic na na kuamini wanaweza kupata kupata ajira ya moja kwa moja katika viwanda hapa nchini kutokana na uhitaji wa wataalam wa aina hiyo kutokana na mabadiliko ya mapinduzi ya viwanda.
Ameongeza kuwa Serikali kupitia chuo cha Veta Kipawa inaweza kupiga hatua na kushindana na wengine katika kutoa vijana wenye umahiri mkubwa shughuli mbalimbali zinazoguza maeneo ya TEHAMA.
Amsema kuwa kutoka na hali hiyo Serikali imwekeza kwa kiwango kikubwa katika miundombinu, vifaa hususan katika vifaa vya kufundishia na kutoa wito kwa wahitimu kusoma zaidi na kuwsa wabunifu ili kufanya mambo makubwa zaidi.
“Pia nakipongeza chuo kwa kufanya mengi mazuri katika kuwanoa vijana wetu ili wakaweze kuewa imara katika soko la ajira na ni vizuri wanapokuwa waondokana na mtazamamo wa kuajiliwa zaidi bali wapambane ili wafungue kampuni zao na waajili vijana wenzao ili kjulisaidia taifa kuondokana na changamoto ya ajira, amesema.
Naye Mkuu wa Chuo hicho Injiania Dickson Sospeter amsema kuwa licha ya juhudi kubwa ambazo wanafanya katika elimu ya mlengwa wa TEHAMA bado wanachangamoto lukuki ikiwemo mbajeti ndogo ya kuendesha shuguli zao za kila na kutoa wito kwa Serikali kuiona namna ya kuweza kuweza kuwasaidia katika kuwaongezea bajeti.
Pia alisema chuo hicho kinauhaba wa hosteli, hivyo ameomba Mamlaka kuweajengea hosteli na tayari eneo ambalo lipo pembezoni mwa chuo hicho limeshapatikana na kinachotakiwa ni kukamilisha mchakato wa ununuzi wa eneo hilo amsema.
Pia Mwakilishi wa wazazi Omari Abdallah, ametoa wito wa wahitimu kuhakikisha wanaitumia vema taaluma ambao wamepata ili kwenda kwenda kuzaliza ajira mpya kwa kufungua kampunji na kuajili wengine na kuachana na dhana na kuajiliwa na kuwaomba pia wasibwetekwe na elimu ambayo wamepata kinachoatakiwa na kuongeza elimu yao ili kujiweka sehemu salama katika ushindani.

No comments:
Post a Comment