MKAKATI SHIKIRIKISHI KULINDA URITHI UKOMBOZI AFRIKA WASUKWA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, January 29, 2024

MKAKATI SHIKIRIKISHI KULINDA URITHI UKOMBOZI AFRIKA WASUKWA


NA SHAMIMU NYAKI

MAKATIBU Wakuu wa Wizara tano wamefanya kikao cha pamoja kujadili mkakati shirikishi wa Kulinda, Kuhifadhi na Kuendeleza Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika uliopo nchini.

Kikao hicho cha Mkakati huo unajadiliwa kwa kuzingatia kuwa Tanzania ndio iliyopewa dhamana ya kuulinda na kuhifadhi Urithi huo na Nchi Wanachama Umoja wa Afrika (AU) mwaka 2011 kupitia azimio la kuanzisha Programu mahsusi ya kuhifadhi kumbukumbu za Ukombozi wa Afrika, kimefanyika leo Januari 29, 2024.


Katika kikao hicho ambacho kimeongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, kimepitia mambo muhimu ili kuhakikisha Tanzania kama mwenyeji wa Urithi wa Ukombozi inakuwa ni ajenda ambayo inashirikisha wadau na kuhakikisha maeneo ya Urithi wa ukombozi yanayopatikana nchini yanaweze kuinufaisha Tanzania na nchi wanachama wa Programu hiyo.


Aidha, lengo la mkakati huo ni kuhakikisha wizara na taasisi ambazo zinahusika kwenye mkakati huo ambazo ni Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Elimu, Maliasili na Utalii, Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ofisi ya Rais -TAMISEMI zinatekeleza Programu hiyo.


Vilevile, kuwa na jukumu la kushiriki, kulinda na kuhifadhi kumbukumbu za Ukombozi ili Kituo hicho kiongeze wigo wa uhifadhi wa Urithi wa Ukombozi wa Afrika.


Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Farasi Mnyepe, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Said Mussa, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Mwingine ni Dkt. Franklin Rwezimula, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Sospeter Mtwale na mwakilishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Antony Mwijage na Wataalamu mbalimbali kutoka wizara hizo.




No comments:

Post a Comment