TANESCO YATEKELEZA KWA VITENDO PROGAMU KUWAJENGEA UWEZO WAHANDISI WANAWAKE KIELIMU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, January 29, 2024

TANESCO YATEKELEZA KWA VITENDO PROGAMU KUWAJENGEA UWEZO WAHANDISI WANAWAKE KIELIMU

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Injinia Gisima Nyamo Hanga, akizungumza  na waandishi wa habari kuhusu programu hiyo.

NA MAGENDELA HAMISI

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeanza kutekeleza kwa vitendo program ya kuwajengea uwezo wahandisi wanawake kwa lengo la kufungua milango ili waweze kuajilika na kujiali wenyewe.

Hayo yamebainishwa leo, Jumatatu Januari 29, 2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Injinia Gisima Nyamo Hanga wakati wa uzinduzi wa progamu hiyo ambayo imeanza na wahandisi wanawake 40 ambao watapiwa elimu kupitia Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) na Chuo cha Dar es Salaam (DIT) kwa kipindi cha miaka minne.

Injinia Nyamo, amesema kuwa mpango huo umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya na wao kama Tanesco dhamira yao ni kuhakikisha baada ya mradi huo kukamilika watauendeleza ili kuongeza idadi ya wahandisi wanawake watakaokuwa na uwezo mkubwa wa kazi na utoa maamuzi katika nyanja hiyo nchini.

“Tukiwa na wahandisi wengi wa kike kwanza itatupa heshima kama Shirika pia itasaidia kuwaajili kwa wingi na wale watakaosa nafasi ya kuajiliwa wanaweza kujiajili wenyewe ama kuajiliwa katika mashirika au kampuni nyingine jambo litakaloongeza ufanisi katika miradi mbalimbali ya umeme nchini,” amesema.

Pia Mnufaika wa program hiyo, Mhandisi Catherine Mwigoha ambaye ni mfanyakazi wa Tanesco wakati akitoa neno la shukrani kwa kupata nafasi hiyo amesema, “Naishukuru  Tansseco na Umoja wa Ulaya kwa kufanikisha hili ambalo kwetu ambao tumepata nafasi tutaitumia ili kuleta tija inayotakiwa ikiwemo kuwemo katika nafasi za maamuzi.

“Hakuna shaka kwamba fursa hii ambayo tumeipata tutaitumia vizuri ili kupata ujuzi wa kutosha utakaotufanya kuwemo katika nafasi za kutoa maamuzi kulingana na uwezo tutakaokuwa nao kwenye utendaji kazi kwa kweli ni jambo la kuishukuru pia Serikali kwa kufanikisha mpango huu adhimu,” amesema.

Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dk. Seif Shekalage, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, amesema programu hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuhakikisha wanawake wanaendelezwa katika elimu kupitia fani mbalimbali.

Ameongeza licha ya kuendelewa kielimu, pia itawasaidia kuwainua kiuchumi kulingana na kipato watakachoweza kupata kulingana na madaraja yao n kazini kiuchumi na kuipongeza Tanesco na kuanza na mchakato huo ambao ni mahusus kuwanua wanawake nchini na kuleta usawa wa kijinsia.

Ameongeza kuwa mwaka Nov. 2023 ilizinduliwa sera wanawake ndani yake imezungumzia mengi kuhusu maendeleo ya wanawake kielimu na kiuchumi na kutokana na mpango huo , Serikali itaendelea kushirikiana bega kwa bega na Tenesco ili kuleta tija kwa kundi hilo.

 

Pia amefafanua kuwa umefika wakati sasa kila taasisi kupanga bejeti kila mwaka kwa ajili ya kuwaendeleza wanawake katika eneo la elimu na mambo mengine ili kuleta uwiano mzuri kijinsia.

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dk. Seif Shekalage, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati kuhusu uzinduzi wa programu hiyo.Mhandisi Catherine Mwigoha ambaye ni mfanyakazi wa Tanesco akitoa akitoa neno la shukrani kwa kupata nafasi hiyo .

No comments:

Post a Comment