NA MAGENDELA HAMISI
WITO umetolewa kwa wanasiasa kuacha kuwazuia wanasheria, viongozi wa dini kutoa maoni yao kuhusu mijadala ya umma ikiwemo inayohusu siasa.
Hayo yamebainishwa leo Feb 15, 2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Taasisi ya Everlastins Legal Aid Foundation )ELAF), Dkt.Hamisi Masoud na kusisitiza kwamba si jambo jema kubaguana kutokana na taaluma kikubwa ni kuangalia vitu gani jamii inapaswa kunufaika navyo kwa maslahi ya taifa.
"Mara nyingi nawaambia wanasiasa kwamba bendera za vyama vyao visiwe na nguvu kuliko Bendera ya Taifa , kitu cha kwanza Mama Tanzania na Baba Tanzania na upendo wetu ni amani, haki na sheria kufuatwa", amesema.
Ameongeza kuwa mtu akiwemo mwanasheria kujinasibu kuwa ni muumini wa chama fulani isiwe sababu ya kubaguana kwa kushindwa kutoa na kupata huduma za kitaalamu kisa unatofautiana kiitikadi ya chama.
Ameongeza kuwa baadhi ya kanuni zinazowaongoza wanasheria ni kutoa huduma za kisheria bila ubaguzi wa aina yoyote na kwenda kinyume ni kufanya dhambi na kuvunja katiba.
Akifafanua kuhusu viongozi wa dini kutakiwa kutojiingiza kwenye siasa, amesema kwamba moja ya kazi ya kundi hilo ni kuhakikisha amani na utulivu inadumu hivyo ikitokea changamoto kwenye siasa kuwazuia kutoa tamko ni kutowatendea haki na kuwanyima uhuru wa kutoa maoni kikatiba.
Dkt. Masoud ameyasema baada ya kuulizwa na Waandishi Habari kama ni sahihi Kwa wanasheria kujihusisha na siasa kama ilivyojitokeza hivi karibuni katika moja ya maandamano ya Chama Cha Siasa kuonekana baadhi ya wanasheria wakionekana kuwa mstari wa mbele kushiriki.
Kutokana na hilo,Katibu Mkuu wa Democratic Party, Abdul Mluya, akadaiwa kajitokeza na kunukuliwa na vyombo vya Habari,akiwashangaa baadhi ya wanasheria kujiingiza kwenye siasa kwa maana wanaweza kushindwa kuwasaidia ipasavyo wananchi wa itikadi tofauti pindi watakapohitaji msaada wa kisheria kwao.
No comments:
Post a Comment