ACT WAZALENDO WAZINDUA SERA YA JINSIA KUCHOCHEA WANAWAKE KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, March 2, 2024

ACT WAZALENDO WAZINDUA SERA YA JINSIA KUCHOCHEA WANAWAKE KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI



NA MAGENDELA HAMISI


CHAMA  Cha ACT Wazalendo kupitia Ngome ya Wanawake, imezindua Sera ya Jinsia ili1 kuchochea kundi hilo kujitokeza kwa wingi kushiriki na kuwania nafasi ya uongozi katika chaguzi na kufikia kwenye ngazi ya maamuzi.


Sera hiyo, imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam katika Mkutano Mkuu wa Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo na Dkt. Ananilea Nkya ambaye ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba na Sheria Tanzania (JUKATA).


Awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Dkt. Nkya kuzindua sera hiyo, Makamu Mwenyekiti Bara wa chama hicho, Doroth Semu, alisema kuwa sera hiyo imekuja ili kuhakikisha mwanamke anafanya vema kwenye siasa na kuepukana na unyanyasaji wa kijinsia.


Amesema kuwa ni hiyo ni sera ya chama ambayo inahitaji mwanamke kuwa imara katika siasa na kuwa usawa wa kijinsia.


"Tunatakiwa kujisifia kwa kufanikisha mchakato huu na kuzindua sera hii itakayosaidia kuleta usawa kijinsia katika chaguzi mbalimbali," amesema. 


Ameongeza kuwa sera hiyo ni nyenzo ambayo inakwenda kutekelezwa katika chama Kwa asilimia zote ili kumpa mwanamke kushiriki na kugombea katika nafasi za uongozi ndani ya chama na kwenye chaguzi za serikali za mitaa.


Ameongeza kuwa chama kinatambua nafasi ya mwanamke na nidhahiri itafanyiwa kazi vema katika kuwajenga wanawake kuhimili kwenye shughuli za siasa.


"Tunahutajij kuona  mwanamke anakombolewa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na utamaduni, amesema. 


Amesema kuwa wanawake wanatakiwa kujenga chama kuanzia chini na kupata wagombea wengi katika chaguzi zijazo.


No comments:

Post a Comment