LHRC : SERIKALI ILETA MSWADA WA MABADILIKO YA KATIBA 2024 - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, April 4, 2024

LHRC : SERIKALI ILETA MSWADA WA MABADILIKO YA KATIBA 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Dkt. Anna Henga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili 4, 2024


NA MWANDISHI WETU

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa wito kwa Serikali kuwasilisha Muswada wa Sheria utakaotoa fursa ya kufanya mabadiliko ya Katiba ili kuruhusu baadhi ya masuala ambayo kwa uasili wake hayawezi kufanyiwa marekebisho bila kugusa Katiba.

 

Hayo yamebainishwa leo April 4, jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Dkt. Anna Henga wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuchambua sheria uchaguzi baada ya kusainiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kupongeza baadhi ya maoni yao ambayo yamefanyiwa kazi.

 

Amesema kuwa wameamua kutoa tamko hilo kwa kuwa LHRC wamehusika kwa njia moja au nyingine kuwasilisha maoni yao mbele ya Kamati ya Bunge ya Uwatawala, Katiba na Sheria jijini Dodoma ili kuboresha mfumo wa Uchaguzi na Vyama Vya Siasa.

 

“Wakati inaletwa miswada hiyo hakika kulikuwa na matumaini mapya kwa taifa letu kutokana na kiu ya muda mrefu kuhusu maboresho ya mfumo wa Uchaguzi na Vyama vya Siasa hapa nchini ingawa tunarejea kutoa rai kwa Serikali kuleta mswada wa mabadiliko ya Katiba, 2024 kwa lengo la kufanya maboresho yanayopendekezwa na wadau na ripoti ya kikosi kazi cha Demokrasia ya vyama vingi iliyowasilishwa na Mwenyekiti wake Prof. Rwekaza Mukandala Oktoba 21, 2022, amesema.

 

Amesema kuwa wamebaini kuwa masuala chanya yaliyomo katika sheria mpya kuna changamoto ya Wakurugenzi wa Halmashauri za Manisapaa, Jiji na Wilaya licha ya kuondolewa kuwa wasimamizi wa Uchaguzi bado wamebaki kuwa waandikishaji wa uchaguzi.

 

Ameongeza kuwa sheria imeweka sifa ya mtu kuwa Msimamizi wa Uchaguzi, Mosi, awe hajawahi kutiwa hatiani katika shauri la nidhamu au kosa lolote la jinai, pili, awe hajawahi kuadhibiwa kwa kifungo kinachozidi miezi sita na tatu, awe hajawahi kuwa kiongozi wa chama cha siasa.

 

Pia amesema sheria imefuta suala la wagombea kupita bila kupingwa katika ngazi zote (Rais, Ubunge na Madiwani) na sharti la Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume kufanyiwa usaili na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji kusimamiwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

 

Pia kufutwa kwa sharti la kulipa ada yakupata upya kadi ya mpiga kura iliyoharibika au kupotea, pamoja na mashauru ya Uchaguzi kusikilizwa ndani ya miezi sita, na nafasi ya kiti cha Ubunge tofauti na pendekezo la miezi 12 kama ilivyokuwa kwenye Muswada.

 

"Hata hivyo mashauru ya Uchaguzi kwa ngazi ya udiwani yatasikilizwa kwa miezi 12 ambayo bado tunaona ni muda mrefu," amesema Dkt. Henga.

 

 

No comments:

Post a Comment