TANZANIA NA DENMARK KUSHIRIKIANA KWENYE AFYA, ELIMU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, April 3, 2024

TANZANIA NA DENMARK KUSHIRIKIANA KWENYE AFYA, ELIMU

 


NA MAGENDELA HAMISI


TANZANIA na Denmark zimeingia makubaliano ya kushirikiana kwenye nyanja ya afya, elimu, biashara na uwekezaji katika maeneo mbalimbali yatakayodumisha ushirikiano ambapo upo kwa sasa. 


Hayo yamewekwa wazi leo, Aprili 3, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya awali kufanya mazungumzo ya pamoja na Waziri wa Denmark anayeshughulikia ushirikiano wa Maendeleo na Sera ya Hali ya Hewa, Dan Jorgensen.

 

Pia amesema kuwa kupitia ushirikiano huo ni dhahiri kila taifa litafanya vema hususan kwenye biashara na kuleta tija stahiki na Denmark watanunua bidhaa mbalimbali kutoka Tanzania na wigo wa uwekezaji utaongezeka


Waziri Makamba amesema kuwa kwa kuwa Denmark wameendelea kiteknolojia, Tanzania itafanikiwa kupata uzoefu katika nyanja mbalimbali na kuongeza kiwango cha biashara na uwekezaji  baina ya mataifa hayo.


 "Katika mazungumzo yetu ya leo tumezungumzia masuala mbalimbali ya kiserikali  na kukubaliana kwa pamoja kushirikiana ili kuleta tija kwa mataifa yetu," amesema.


Pia amesema kuwa watashirikiana kwenye masuala ya siasa kwa lengo la kukuza demokrasia ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi hizo.


Ameongeza kuwa ni urafiki wa Tanzania na Denmark ulianza siku nyingi na umekuwa ukichanua kila kukicha jambo ambalo linaendelea kujenga historia nzuri ya ushirikiano.


Ametanabaisha kuwa mwaka 2021 taifa hilo lilifunga ubalozi wake hapa Tanzania na mwaka jana, iliondoa uamuzi huo na kuufungua tena jambo ambalo kwa Tanzania ni faraja.


"Kwakweli kuona wenzetu wameamu kwa dhati kabisa kuugua tena ubalozi wao nasi tunafuraji kwa hilo kwa maana inaendelea kudumisha mahosiano yetu yalijengeka tangu uhuru na hatupendi kuona ukitetereka," amesema.


 Amefafanua kuwa pia  wamezungumzia siasa za kimataifa ambapo Denmark inatarajia kuwa Mjumbe wa Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa na Tanzania inaunga mkono kuwa na imani kuwa watakapokuwa humo maslahi ya nchi za Afrika na Tanzania yatazingatiwa.

Naye  Waziri  wa  Denmark,  Jorgensen alisema wamezungumzia mashirikiano kwa pande  zote  mbili  katika masuala  mbalimbali  ikiwemo  afya na elimu pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi.

No comments:

Post a Comment