NA MWANDISHI WETU, TABORA
MAHAKAMA ya Mahakama ya Wilaya ya Tabora Leo, Aprili 25, 2024 Mbele ya Mhe. Demetrio Nyakunga, imefunguliwa kesi ya uhujumu uchumi No.10892/2024 - Jamhuri dhidi ya MICHAEL FREDRICK MGONGO (Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Uhazili Tabora).
Kesi hii ilikuja kwa kusoma hati ya mashtaka kwa mshtakiwa ambapo mshtakiwa alikana kosa lake.
Mshtakiwa anashtakiwa kwa kosa la kuomba rushwa ya ngono toka kwa mwanafunzi wake kosa ambalo ni kinyume na k/f cha 25 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 Rejeo la 2022.
Mshtakiwa yuko nje kwa dhamana na shauri limepangwa kusoma hoja za awali na kusikilizwa - Mei 23, 2024.
No comments:
Post a Comment