WAKILI, MFANYABIASHARA WAPANDISHWA KIZIMBANI WAKIDAIWA KUGUSHI NYARAKA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, April 25, 2024

WAKILI, MFANYABIASHARA WAPANDISHWA KIZIMBANI WAKIDAIWA KUGUSHI NYARAKA


NA MWANDISHI WETU 

LEO Aprili 25, 2024 katika Mahakama ya Wilaya Ilala limefunguliwa shauri la Uhujumu Uchumi namba 10936/2024 mbele ya Mhe. Rehema Lyana-Hakimu Mkazi Mwandamizi, ambapo washtakiwa, David Andindilile ambaye ni Wakili wa kujitegemea na Hamza Suleiman Rajabu ambaye ni mfanyabiashara  wamesomewa jumla ya mashtaka 14 ya Kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo na Utakatishaji fedha haramu.


Makosa haya ni kinyume na Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura 16 marejeo ya 2023 pamoja na Sheria ya Kuzuia Utakatishaji Fedha Sura 423 marejeo ya 2023.


Washtakiwa hao wamekana makosa yao na kupelekwa mahabusu kutokana na kukosa vigezo vya dhamana.


Aidha mshtakiwa Daniel Stanford Semwenda katika kesi hiyo, hakusomewa mashtaka yake kwa kuwa anaishi Nje ya Nchi na juhudi za kumtafuta ili ashtakiwe zinaendelea.


Kesi imeahirishwa hadi Mei 9, 2024 kwa ajili ya hoja za awali.

No comments:

Post a Comment