PROF.GURNAH ATUA DAR, KUSHIRIKI TUZO YA TAIFA YA UANDISHI BUNIFU - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, April 12, 2024

PROF.GURNAH ATUA DAR, KUSHIRIKI TUZO YA TAIFA YA UANDISHI BUNIFU


NA ANDREW CHALE

MWANDISHI Mkongwe wa vitabu Prof. Abdulrazak Gurnah ametua jijini Dar es Salaam, ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika usiku wa tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu ambayo itafanyika Aprili 13, 2024 katika ukumbi The Super Dome, Masaki.


Tuzo hizo ambazo zitafanyika siku ya kumbikizi  ya kuzaliwa Mwalimu Julius Nyerere na mwaka huu ni za msimu wa pili zikiwa zinaratibiwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) chini ya uangalizi wa Wizara ya Elimu. 


Akizungumza na katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Prof. Gurnah ameeleza; 

“Ni heshima kubwa kualikwa kuja kuungana katika sherehe hii ya tuzo ya Nyerere kuwasaidia waandishi wenzangu, lakini pia kuja nyumbani kuonana na ndugu na jamaa.’’ Amesema Prof. Gurnah


Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda wakati wa kumpokea mgeni huyo amemshukuru Prof. Gurnah kwa kukubalia mwaliko huo kwani ni heshima ya kipekee kwa washiriki  wabunifu wa tuzo hizo kukutana na mwandishi huyo nguli.


Aidha, katika tukio hilo la mapokezi, Waziri wa Elimu Prof. Mkenda aliambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba na wafanyakazi wa TET na wadau mbalimbali.



No comments:

Post a Comment