SERIKALI YATAKIWA KULIKAGUA BARAZA LA WAFUGAJI KUFAHAMU MATUMIZI YA SHILINGI BILIONI 22. - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, April 21, 2024

SERIKALI YATAKIWA KULIKAGUA BARAZA LA WAFUGAJI KUFAHAMU MATUMIZI YA SHILINGI BILIONI 22.


NA MWANDISHI WEU

BAADHI ya wajumbe wa Baraza la Wafugaji Tarafa ya Ngorongoro (NPC) wameiomba serikali kufanya ukaguzi maalum matumizi ya fedha ya  baraza hilo ili kuondoa mgogoro wa chini kwa chini uliopo baina ya viongozi wa baraza hilo na wajumbe wake.


Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wajumbe wa baraza hilo kufuatia tuhuma walizoeleza kuwa kumekuwa na ulaji mkubwa wa fedha za baraza kinyume cha taratibu za matumizi ya fedha.


Wajumbe hao hawakutaka majina yao wameeleza kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita baraza lilipokea zaidi ya shilingi bilioni 22  kutoka vyanzo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi lakini hakuna uwazi wowote katika matumizi ya fedha hizo.


"Baraza hili limeanzishwa ili wajumbe wote tunufaike nalo pamoja na wananchi tunaowaongoza lakini wamekuwa wakifaidika watu wachache kwa safari za hapa ana pale huku wengi wetu tukikosa hata posho hasa pale tunapohudhuria vikao mbalimbali hali inayotufanya tuishi katika mazingira magumu katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku”,alisema mjumbe mmoja wa baraza hilo.


Wameongeza kuwa viongozi wao wanakiri kupokea fedha kutoka ndani na  nje  ya nchi zaidi ya shilingi bilioni 22 lakini hakuna anayejua mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo zaidi ya watu wachache inaoelezwa kuwa shilingi bilioni 12.5 zimetumika kwa safari za viongozi wa juu kutoka Karatu kwenda Arusha, Dar es salaam na Nairobi nchini Kenya.


Pia inadaiwa kuwa mmoja wa kiongozi wa juu wa baraza hilo ametumia takribani shilingi milioni 6 za baraza hilo kwa ajili ya kumlipia ada mtoto wake anayesoma nchini Uganda kitu ambacho ni kinyume na taratibu za baraza hilo.


Juhudi za kumpata Msajili wa Taasisi zisizo za kiserikali katika mkoa wa Arusha kuelezea kuhusiana na uendeshaji wa baraza hilo kwa sasa hazikuweza kuzaa matunda baada ya simu yake kutopatikana huku viongozi wa baraza hilo nao wakishindwa kupatikana.

No comments:

Post a Comment