WAMACHINGA KARIAKOO WATAKIWA KUSHIKAMANA, KUCHAGUANA APRIL 19 - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, April 12, 2024

WAMACHINGA KARIAKOO WATAKIWA KUSHIKAMANA, KUCHAGUANA APRIL 19



NA MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Chama Cha wafanayabiashara wadogo ( Wamachinga) Mkoa wa Dar es salaam ( KAWASO), Steven Lusinde amewasihi wanachama wa chama hicho kushikamana , kupendana na kuwa wamoja katika kuendeleza maendeleo ambayo yamefikiwa tangu ilipoanzishwa mwaka 2017.


Lusinde ametoa nasaha hizo hivi karibuni katika Mkutano Mkuu wa kikatiba wa chama hicho ulifanyika katika Ukumbi wa Sabasaba jijini Dar es Salaam nakubainisha kuwa kuna baadhi ya wanachama wameanza kutumika vibaya na baadhi ya wanasiasa wenye nia ovu ya kuwachafua viongozi wa KAWASO kwa maslahi yao binafsi.

"Tushirikiane kujenga kawaso yetu, sisi tumetoka katika mazingira ambayo hayaeleweki kabisa,lakini kwasasa tulipotoka,tulipo na tunakoelekea tumepiga hatua kubwa za mafanikio tusikubali kufarakanishwa na watu ambao wanataka maslahi yao binafsi"amesisitiza Lusinde 


Amesema kuwa Maisha ya Wamachinga wa Kariakoo yapo mikononi mwao hivyo wakikosea kuwasikiliza wale wanaotaka kubomoa chama chao watakua wameshindwa kupata fursa zao za kimaendeleo ambazo kwa sasa zimeanza kujitokeza chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan


Lusinde kupitia Mkutano huo ametangaza kuwa Mkutano maalumu wa uchaguzi wa viongozi wa KAWASO utafanyika April 19 , 2024 huku akiwasisitiza wanachama kuchagua viongozi wenye maono ya kukifikisha mbali chama hicho.


"Viongozi ambao watachaguliwa April, 19 2024 wawe ambao kauli yao ya pamoja ni kutengeneza Kariakoo ya pamoja, Kariakoo ya upendo,mshikamano na kufikia ndoto za maendeleo yetu" amesema Lusinde.


Awali akisoma taarifa ya mafanikio na changamoto tangu kuanzishwa kwa chama hicho, Mwenyekiti wa KAWASO, Namoto Yusuph Namoto amesema hadi sasa wamepata mafanikio makubwa licha ya kuwepo baadhi ya watu wanaobeza mafanikio hayo.


Amesema KAWASO imefanikiwa katika mambo mbalimbali ikiwemo kuondoa migogoro kati ya Machinga na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya, kuwa na kanzi data ya kuwatambua wamachinga, kupata vitambulisho vya NIDA na TRA , kupata mikopo ya mitaji na viwanja kutoka taasisi za kifedha ikiwemo Benki ya Maendeleo, pamoja na kuhakikisha utunzaji wa mazingira unatekelezwa ipasavyo.


Namoto pia amesema mafanikio yamekuwa mengi na changamoto kubwa inayoikabili chama hicho ni kukosekana kwa vyanzo vya mapato, ambapo amewashauri wanachama washikamane kuanzisha vyanzo hivyo akitolea mfano SACCOS ili kusaidia kujiwezesha wenyewe kupata mikopo bila riba.


Katika hatua nyingine Namoto amewasisitiza wamachinga kumuunga mkono rais Dkt Samia Suluhu Hassan kulinda amani na kuacha kutumika na watu wenye nia ovu ya kuvunja amani ya Taifa la Tanzania ambalo linasifika kwa tunu za amani, mshikamano na upendo.


" Sisi haya ndio maisha yetu, tuache kutumika vibaya wale wanaotaka tuvunje amani yetu hatuko tayari kufanya hivo, tumekua tukifanya makongamano ya amani katika moja ya mafanikio yetu mfano tarehe 25, 10, 2023 tulifanya pale viwanja vya mashujaa ikiwa lengo ni kuunga mkono serikali ya Dkt Samia ambaye anapenda maridhiano na sio machafuko kwenye taifa letu.


Mkutano huo umehudhuriwa na wanachama zaidi ya elfu mbili(2000) huku wanachama  hao wakionyesha kuwa na matumaini makubwa na uongozi uliopo baada ya kuzungumza na chombo hiki cha habari kwa nyakati tofauti.




No comments:

Post a Comment