ZAIDI YA WATOTO 50 WENYE VICHWA VIKUBWA NA MGONGO WAZI WAHUDHURIA KLINIKI YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI MOI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, April 13, 2024

ZAIDI YA WATOTO 50 WENYE VICHWA VIKUBWA NA MGONGO WAZI WAHUDHURIA KLINIKI YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI MOI


NA ABDALLAH NASSORO, MOI

ZAIDI ya watoto 50 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wamehudhuria kliniki maalum ya uchunguzi na utambuzi kwa ajili ya kambi ya upasuaji ya Aprili 20, 2024 inayofadhiliwa na Taasisi ya MO Dewji Foundation.


Daktari bingwa mbobezi wa ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu wa MOI Dkt. Hamisi Shabani amesema zoezi hilo limefanyika kwa mafanikio makubwa na linatoa taswira ya kufanyika kwa kambi maalum ya upasuaji kwa njia ya matundu mapema wiki ijayo.


“Zoezi hili limeenda kwa mafanikio makubwa na sisi MOI ndiye kituo cha umahiri kwa tiba za watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi na kwasasa tunatumia teknolojia ya kisasa ya upasuaji kwa njia ya matundu, teknolojia ambayo  inakupa uhakika wa matokeo chanya” amesema Dkt. Shabani 


Amefafanua kuwa “Tatizo hili ni kubwa hapa nchini, inakadriwa watoto 6,000 huzaliwa wakiwa na tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi, wengi hukimbilia kwa waganga wa kienyeji na wanaambiwa huo ni mkosi, mwanaume anakiambia famialia na kuacha mzigo wa malezi kwa akina mama pekee,


…tunaishukuru Mo Dewji Foundation pamoja na chama za wazazi wenye watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi ASBATH kwa ushirkiano huu muhimu” 


Amesema tatizo la vichwa vikubwa na mgongo waazi husababishwa na mama kukosa madini ya frolic acid kabla na wakati wa ujauzito  na kwamba jamii inaweza kuepukana nalo kwa akina mama kula vyakula vyenye madini hayo.


Mfanyabishara Mohammed Dewji (Mo Dewji) ambaye leo Aprili 13,2024 ametembea katika zoezi hilo la utambuzi na kupata fursa ya kuwafariji watoto wenye matatizo hayo na wazazi wao.


“Nawaombea kwa mwenyezi Mungu, Mungu awape subra, inshallah naomba asaidie lipite hili jambo watoto wetu wapate nafuu na waweze kuanza maisha yao mapya, mimi nawapeni pole huu ni mtihani lakini Mwenyezi Mungu anasema akikupa mtihani lazima akupe moyo wa kuvumilia huo mtihani, tusichoke tuzidi kumuomba zaidi” amesema Dewji 


Mkurugenzi wa chama cha wazazi wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi (ASBATH) Suma Mwaipopo licha ya kuishukuru taasisi ya MO Dewji Foundation amesema bado jitihada kubwa zinahitajika kuelimisha jamii juu ya kujikinga na tatizo hilo.


Kwa upande wake mmoja wa wazazi wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi, Mabuga Bandondaki Karigilwa ameishukuru taasisi ya MO Dewji Foundation kwa msaa huo wa matibabu na kwamba matibabu ya watoto hao yamekuwa na gharama kuwa hali inayochangia kukosa matibabu.



No comments:

Post a Comment