BRELA YAPATA TUZO TAASISI BORA KIDIGITALI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, May 25, 2024

BRELA YAPATA TUZO TAASISI BORA KIDIGITALI


NA MWANDISHI WETU

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imepata tuzo katika kipengele cha taasisi bora ya  Serikali kidigitali ikiwa ni kutambua mchango bora katika mageuzi ya kidigitali nchini Tanzania.


Tuzo hizo zimeandaliwa chini ya programu iitwayo Funguo Innovation inayosimamiwa na UNDP kwa kushirikiana na Kampuni ya Serengeti Bytes na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) yenye lengo la kutambua michango mbalimbali inayotolewa na Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi nchini katika utoaji wa huduma kwa jamii. 


Tuzo za Kidigitali kwa mwaka 2024 zilienda sambamba na maadhimisho ya miaka 10 ya wiki ya ubunifu ikiangazia mafanikio na changamoto katika ubunifu wa kidigitali.

No comments:

Post a Comment