VIONGOZI WAKUTANA KUJADILI MAANDALIZI YA CHAN 2024 NA AFCON 2027 - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, May 6, 2024

VIONGOZI WAKUTANA KUJADILI MAANDALIZI YA CHAN 2024 NA AFCON 2027


NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Damas Ndumbaro ameongoza kikao cha kujadili maandalizi ya Fainali za Mashindano ya CHAN mwaka 2024 na AFCON 2027 yatakayofanyika nchini Tanzania kwa kushirikiana na Kenya na Uganda  kilichofanyika leo Mei 6, 2024 Jijini Dodoma.


Kikao hicho kimejadili  ukarabati wa miundombinu ambayo itatumika katika mashindano hayo iliyopo Tanzania Bara na Zanzibar kwa kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na Wakaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).


Kikao hicho  kimehudhuriwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Mwita, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Fatma Hamad Rajab, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Suleiman Serera, baadhi ya watendaji wa wizara na viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiongozwa na Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia.

No comments:

Post a Comment