NDUMBALO MGENI RASMI TAMASHA LA GRAND GALA DANCE - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, July 24, 2024

NDUMBALO MGENI RASMI TAMASHA LA GRAND GALA DANCE


NA MAGENDELA HAMISI

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Damas Ndumbalo anatarajiwa mgeni rasmi katika tamasha la Grand Gala Dance linatakalofanyika Agosti 30 mwaka huu katika Ukumbi wa Super Dom, Masaki jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa kampuni inayoandaa tamasha hilo la Muziki wa Dansi nchini kwa msimu wa tatu, Chocolate Princess,  Mboni Masimba, amesema siku hiyo bendi nne zitafanya onesho la pamoja. 

"Bendi ambazo zitafanya onesho hilo ni FM Academia chini ya Patcho Mwamba, African Stars Twanga Pepeta chini ya Charles Baba, Malaika Bendi na Tukuyu Bendi,"amesema.

Mwakikishi wa CRDB Benk, Sauda Makila ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara, amesema kuwa wamejiandaa kutoa huduma.mbalimbali ikiwemo kulipia tiketi kwa njia ya mtandao.

"Tumejipanga vizuri katika huduma ZOTE ,a kibenki hususan wenye akaunti ya CRDB, hivyo nawaomba mashabiki wote waje Kwa wingi," amesema

No comments:

Post a Comment