UVCCM WAKABIDHIWA VIFAA VYA KILIMO VYA MIL 200 - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, July 19, 2024

UVCCM WAKABIDHIWA VIFAA VYA KILIMO VYA MIL 200

 


NA MAGENDELA HAMISI

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM imekabIdhiwa vifaa vya Kilimo vyenye thamani ya Shilingi 200.

Mwenyekiti wa UVCCM, Ally Kawaida amepokea vifaa hivyo leo, Julai 19, 2024 jijini Dar es Salaam kutoka kwa taasisi ya ujenzi wa Sayansi ya Changzhou ya nchini China, (Changzhou Building Science Institute (CBS).

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Kawaida amesema kuwa hayo yamekuja kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan, kufungua milango ya uwekezaji kwa wawekezaji wa Kimataifa kuja nchini na kutanua fursa za kiuchumi hususan kwa vijana wa kitanzania bila kujali chama. 


"Vifaa hivi vimekuja si kwa bahati mbaya, unatokana na udugu wetu wa damu ulioasisiwa miaka mingi na viongozi na udugu huu si wa kwenye makaratasi, mtakumbuka wakati nchini hizi mbili zinapambana kujijenga kiuchumi, wenzetu hawa walitusaidia kufungua mipaka yetu kwa kujenga njia ya reli ya Tazara," amesema. 

Pia amesema tayari amezungumza na kamati husika ndani ya Jumuia hiyo ya vijana ili kuweka utaratibu mzuri wa kutumia vifaa hivyo ili kuhakikisha vinatumia ipasavyo kwa ajili ya kuinua uchumi kupitia Kilimo.

Naye Katibu Mkuu wa UVCCM, Joketi Mwegelo, amesema anashukuru kwa Jumuia hiyo kupata vifaa  hivyo na nidhairi, wanakwenda kufanya vizuri katika kuinua uchumi wa vijana wa Kitanzania kupitia Kilimo.

"Tayari tumepokea maelekezo ya Mwenyekiti wetu ya kupanga utaratibu wa namna ya kutumia vifaa hivyo ili kuleta tija Kwa vijana wa kitanzania  hususan wenye uhitaji kwenye nyanja ya Kilimo hapa nchini," amesema.

Meneja wa Kampuni ya Amec ya nchini China, ambayo imetoa vifaa hivyo, Jason Xiong Jun, amesema wamejipanga kuja kuwekeza hapa Tanzania na wametoa vifaa hivyo Kwa ajili ya kusaidia kujenga uchumi Kwa watanzania kupitia Kilimo.

"Leo ni siku njema kwetu Kwa kuendeleza ushirikiano wetu katika sekta hii, pia katika nyanja ya kilimo tunauzoefu wa miaka 40, hivyo naamini tutafanikiwa," amesema


Pia Mwenyekiti wa CBS, Yang Jiangjin amesema kwamba hapa nchini watafanya tafiti za kisayansi katika mikoa ya mikoa ya Kanda Mashariki.

"Kutokana na tafiti hizo tutaweza kusaidia kuondoa changamoto zilizoko katika nyanja hiyo," amesema.


No comments:

Post a Comment