DKT MGONJA AWATAKA WAKULIMA KUTUMIA MBEGU ZA TANZANIA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, August 2, 2024

DKT MGONJA AWATAKA WAKULIMA KUTUMIA MBEGU ZA TANZANIA


NA MONICA SIBANDA, DODOMA

MKURUGENZI wa Kampuni ya Namburi Agricultural Company ambao ni wazalishaji wa mbegu bora Dkt Mary Mgonja amewataka wakulima nchini kutumia mbegu zinazozalishwa nchini ambazo zinaviwango na zinahimili ardhi aina zote.


Akizungumza na waandishi wa Habari leo Augost 2,2024 kwenye maonesho ya Kimataifa ya wakulima Nanenane Mkoani Dodoma amesema kampuni yao imekuwa ikizalisha mbegu zenye ubora lakini pia zinahimili mpaka kwenye ukame.


"Hapo sisi tunambegu mpaka zinazohimili kwenye ukame mbapo mkulima wa maeneo hayo anaweza kuzitumia na akafanikiwa kuvuna vizuri na kufanyabiashara",Amesema Dkt Mgonja.


Aidha ameipingeza Wizara ya kilimo kwa kushirikiana na Tosci kwa kuitangaza nchi lakini pia kuzuia uuzaji wa mbegu bandio.


"Nitoe rai kwa wakulima pia kuwa makini wakati wa kununua mbegu kuhakikisha mbegu hizo zina alama ya Tosci",Amesema.


Ameongeza Kampuni ya Mamburi inafanya shughuli zake za uchakataji na uzalishaji katika Mkoa wa Songwe na wanasambaza mbegu zao kwenye maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha kila mkulima anapata mbegu hizo.


 Dkt Mgonja pia amewata wastaafu kutumia muda huo wa kuingia kwenye kilimo ili kuendelea kufanyakazi na kujiimarisha kiafya na kiuchumi.




No comments:

Post a Comment