WANANCHI WATAKIWA KUTEMBELEA BANDA LA TRA KUPATA ELIMU KWENYE MAONESHO YA NANENANE - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, August 2, 2024

WANANCHI WATAKIWA KUTEMBELEA BANDA LA TRA KUPATA ELIMU KWENYE MAONESHO YA NANENANE


NA MONICA SIBANDA, DODOMA

MAMLAKA ya Mapato Tanzania TRA imetoa rai kwa wakulima na wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye banda lao ili kupata elimu ya kodi lakini pia kufahamu bidhaa za kilimo zilizo kwenye msamaha wa kodi.


Wito huo umetolewa leo Agost 2,2024 mkoni Dodoma kwenye viwanja vya maonesho ya nanenane vilivyopo Nzuguni na Afisa msimamizi wa kodi Philip Eliamini wakati akizungumza na waandishi wa habari.


Amesema wamejikita kutoa elimu ya kodi kwenye maonesho hayo kwani wakulima ni wadau wazuri wa kodi na serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa ili kumuwezesha mkulima kulima kibiashara na kuweza kulipa kodi.


"Nawasihi wakulima wafike kwenye viwanja hivi ili waweze kujifunza na kupata elimu ya msamaha kodi kwa dhana za kilimo zilizopo kwenye msamaha huo",Amesema.


Sambamba na hayo Eliamin amesema pia wanatoa huduma ya namba ya mlipa kodi (TIN NAMBA) kwa watu ambao awana lakini wanatoa huduma ya ukadiliaji kodi kwa wafanyabiashara.


Pia amesema kila mfanyabiashara mwenye mauzo ya milioni 11 kwa mwaka anapaswa kutumia mashine ya EFD.


Aidha ameongeza kuwa maagizo yaliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara Uvuvi na Mifugo, Profesa Shemdoe watayafanyia kazi na amewataka wadau pia kuyafanyia kazi.

Pia amewataka wadau wanaoagiza bidhaa zilizo kwenye msamaha  kodi kuwasilisha nyaraka zao kwa TRA mapema  kabla ya bidhaa hizo kufika huku pia amewataka watendaji wa TRA kufanyakazi kwa bidii na weledi.

No comments:

Post a Comment