NA HALIMA MWAMBA
MCHUNGAJI wa Taifa, Nabii Nikaya Komando Mashimo, amesema kwamba wanajipanga kukata rufaa kutokana na kufungwa kwa Kanisa la Kiboko ya Wachawi.
Hayo amebainisha leo Agosti 2, 2024 katika Kanisa hilo, Buza jijini Dar es Salaam na kubainisha kinachotakiwa sasa kwa Msajili kuweka wazi changamoto nyingine tofauti na iliyoelezwa kuwa mchungaji huyo amefungiwa kutokana na kutoza fedha waumini ili kupata huduma.
"Huduma hii ambayo ilikuwa inatolewa hapa ilikuwa ikiponya waumini wengi na kubadilisha maisha ya watu, wapo baadhi ya waumini wamekuwa wakihudumiwa bure, hivyo ombi letu ni kuiomba Serikali kuangalia upya jambo hili," amesema.
Pia ametoa wito wananchi na wadau wengine wasihusishe kufungiwa kwa kanisa hilo na Serikali, kama maana iliyofungia taasisi.
Pasta Anna sunza, amesema kuwa tangu amefika katika kanisa hilo, amepona maradhi ya moyo ambayo yamekuwa yakimkabiri kwa kipindi kirefu.
Ameongeza kuwa si kweli kwamba Mchungaji wao ni tapeli kama ambayo inasemwa na baadhi ya watu.
Pia Mama Ntilie ambaye anauza biashara ya chakula pembezoni mwa kanisa Hilo, Shukani Ismael, anasema kuwa uwepo wa Kanisa Hilo umesaidia kupunguza uhalifu ukiwemo wizi, utumiaji wa dawa kulevya, ukabaji.
"Kwa kweli wizi ulikuwa umepungua Sana, sasa sijui hali itakuwaje baada ya kufungiwa kwa kanisa, hivyo naomba Serikali iangalie kwa huruma, ila Luna mengine waweke wazi," amesema.
No comments:
Post a Comment