RAIS wa Jamhuri wa Muungano Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan,anatarajiwa
kuhutubia katika Mkutano wa Tisa wa Kilele wa Wakuu Nchi na Jukwaa la Ushirikiano
kati ya China na Afrika (FOCAC) utakaoanza Septemba 4 hadi 6 mwaka huu katika
Jiji la Beijing nchini China.
Hayo yamebainishwa leo Agosti 31, 2024 jijini Dar es Salaam na
Waziri wa Mambo ya Ndani na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mahamoud Thabit Kombo
wakati akizungumza na waandishi wa Habari kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa
kushika nafasi hiyo na kubainisha kuwa Rais Samia katika mkutani huyo ataongoza
ujumbe wa watu wa tano kutoka Tanzania.
“Rais Samia anashiriki mkutano huo baada ya kupata mwaliko
kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping, na hayo ni mafanikio
makubwa kwa Tanzania na unaendeleza ushirikiano ambao unatimiza miaka 60 tangu
kuasisiwa kwake,” amesema.
.Ameongeza kuwa katika mkutano huo Tanzania na China zitawekeana
saini ya kufanya maboresho ya reli ya Tazara ili kuifanya kuwa na ubora wa hali
ya juu na kuanza kutumika mabehewa ya kisasa kutoka hapa Tanzania hadi Zambia
jambo litakaloimarisha usafiri wa njia ya reli.
Amefafanua kuwa katika mkutani huyo Tanzania pia itajikita katika
majadiliano katika nyanja mbili ya kilimo na uchumi wa viwanda ambayo itatoa
fursa katika sekta ya uwekezaji ambayo ndio mahusus kwa sasa.
Ameongeza
kuwa,utasaidia kuibua fursa mpya za ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili
pamoja na kutangaza maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya Sita
ya sera na sheria katika sekta ya biashara na uwekezaji ili kuvutia wawekezaji
wengi zaidi kutoka nchini humo.
Amebaisha
kuwa Kaulimbiu katika mkutano huo ni “Kushirikiana ili Kuendeleza Usasa na
Kujenga Jamii Bora ya China na Afrika kwa Mustakabali wa Pamoja" na tayari
mataifa 40 kati ya 54 ya Afrika yamethibitisha kushiriki hadi sasa.
Jukwaa la FOCAC lilianzishwa mwaka 2000 na Jamhuri ya Watu wa
China kwa lengo la kukuza ushirikiano na maendeleo ya pamoja kati ya China na
Afrika, ambapo tangu kuanzishwa kwake jumla ya mikutano ya Kilele (Wakuu
wa Nchi na Serikali) nane imefanyika na inafanyika kila baada ya miaka mitatu.
Ameongeza kuwa mkutano huo wa tisa utafunguliwa na Rais wa China
Jinping na atatoa hotuba yake ya ufunguzi itakayotoa uelekeo wa China katika
uhusiano wake na nchi za Afrika,
Mkutano
huo utawakutanisha viongozi na wakuu wan chi za Afrika, wawakilishi wa
mashirika ya kikanda ya Afrika, mashirika ya kimataifa na wadau wengine
walioalikwa.
Baadhi ya viongozi walioalikwa na wanaotarajiwa kushiriki katika
mkutano huo ni Antonia Guterres ambaye ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Moussa
Faki ambaye ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Rais wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika.
Balozi Kombo amefafanua kwamba katika mkutano huo mada
zitakazojadiliwa ni nne ambazo ni Utawala wa Nchi, Mpango wa Miundombinu na
Uwekezaji, Maendeleo ya Viwanda na Kilimo cha Kisasa na Amani na Usalama, kwa
upande wa Tanzania utajikita kwenye mada ya Maendeleo ya Viwanda na Kilimo kutokana
na kuzingatia Mpango wa Maendeleo wa Tatu wa Miaka Mitano, ambao ndiyo mpango
wa mwisho wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Tanzania ya 2025.
Amesema
Tanzania inatarajia kuwasilisha miradi mbalimbali ikiwemo mipya na ile ambayo
haiweza kutelezwa kwenye mpango uliopita wa FOCAC kwa sababu mbalimbali, ili
iweze kutekelezwa chini ya mpango kazi wa FOCAC kwa kipindi cha 2025-2027 kwa
kupatiwa fedha za mkopo nafuu na msaada.
Miradi
hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Mtandao wa Mawasiliano Vijijini wa awamu ya pili,
Ujenzi wa njia ya kusafirisha Umeme wa Kv 400 wa awamu ya Pili na Tatu , Ujenzi
wa Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) wa awamu ya Pili na Ujenzi wa Babara za
Zanzibar Zenye Urefu wa Kilomita 277.7 .





No comments:
Post a Comment