NA MWANDISHI WETU
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Kinondoni imesema kuwa utoaji wa elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi ya taka imesaidiia ongezeko la mapato na kuwa wastani wa milioni 400 kwa mwezi kutoka wastani wa milioni 380.
Hayo yamebainishwa leo na Naibu Mkuu Takukuru Mkoa wa Kinondoni, Elizabeth Mokiwa alipokuwa akiwasilisha kwa Waandishi wa Habari, taarifa ya miezi mitatu ya utendaji kazi ya taasisi hiyo kuanzia Aprili 2024 hadi Juni mwaka huu.
“Utoaji wa elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi ya taka ambao umefanyika kupitia kampeni ya ‘Mguu kwa Mguu’, ‘Chocho Kwa Choho Kitaa’ chini ya usimamizi wa watendaji Kata, Ofisa Usafirishaji wa Manispaa na Wakandarasi imesaidia kusikilizwa na utatuzi wa kero kuhusu uzoaji taka na kufanikisha ongezeko la wastani wa sh. mil. 400 kwa mwezi kutoka mil. 380 za usafi wa mazingira,” amesema.
Ameongeza kuwa katika kufanikisha mafanikio hayo, Takukuru Mkoa wa Kinondoni hufanya vikao na wadau mbalimbali na kuwekeana na maazimio jambo linalosaidia wepesi wa ufuatiliaji wa mchakato huo.
Pia amesema hatua hiyo imekuja kutokana na kuwepo kwa maazimio hayo na ufuatiliaji wa kina ambapo wamebaini kwamba wananchi wamepewa elimu ya kutosha kuhusu, utumiaji wa mashine za EFD na kufanikisha kiwango sahihi cha fedha ya kodi ya zuio kinachostahiri kukatwa.
“Mchakato huo umesaidia kodi ya zuio kukatwa na kuwasilishwa katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa wakati kama tulivyoazimia kwenye vikao na wadau wa uwasilishaji wa kodi ya zuio, katika ununuzi wa vifaa na huduma katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni,” amesema.
Pia amesema maazimio mengine ambayo yamefanyiwa kazi ni Local mafundi wote wa Manispaa ya Kinondoni anayepewa kazi alishauriwa kuwa na TIN Namba lengo likiwa kusaidia kodi kukusanywa kama inavyotakiwa na kuinua mapato ya ndani na kukamilika miradi kwa wakati.
mwisho
No comments:
Post a Comment