TAKUKURU KINONDONI YAJIPANGA KUTOA ELIMU YA RUSHWA KIPINDI CHA UCHAGUZI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, August 5, 2024

TAKUKURU KINONDONI YAJIPANGA KUTOA ELIMU YA RUSHWA KIPINDI CHA UCHAGUZI


NA MAGENDELA HAMISI

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Kinondoni imejipanga kuwaelimisha wananchi katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani ili wafahamu kuwa madhara rushwa.

Hayo yamezungumzwa jana jijini Dar es Salaam, Agosti 5, 2024 na Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni, Elizabeth Mokiwa wakati akitoa taarifa wa wanahabari ya miezi mitatu ya utendaji kazi wa taasisi hiyo kuanzia April 2024 hadi Juni mwaka huu .

Katika kipindi hiki cha miezi mitatu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,  Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa kwa pamoja tulishiriki katika kongamano la vijana wapatao 949 wakati wa maadhimisho ya Mbio za Mwenge katika viwanja vya Bunju A.

Amesema kongamano hilo lilifanyiika Mei 11, 2024 lilihusisha vijana waliopo Manispaa ya Kinondoni na waliovyuoni wilayani Kinondoni, Shule za Msingi na Sekondari pamoja na kutoka vyama vya siasa na mgeni rasmi alikuwa Godfrey Mnzava.

Mokiwa ameweka wazi kuwa katika kongamano hilo, Mnzava alitoa wito kwa Manispaa ya Kinondoni kuhakikisha inatoa elimu na hamasa kwa vijana na jamii kwa ujumla kuhusiana na maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Katika kongamano hilo, Mnzava alisisitiza kuwa kuna vituo 1630 vya kupigia kura, hivyo wadau na viongozi washughulikie kuhakikisha vijana wanakuwa mstari wa mbele kwenye kila hatua za uchaguzi,” amesema.

Pia ametoa wito kwa wanancho wote katika mkoa huo wa Kinondoni kuendelea kutoa ushirikiano kwa TAKUKURU na kuwasishi kuwa wapatapo taarifa zozte zinazohusu, rushwa wawasiliane nao bure kwa kupiga au kutuma ujumbe mfupi kwa namba ya dharura 113 na kufuata maelekezo au kwa kufika ofisi yoyote iliyopo karibu.

  

No comments:

Post a Comment