NA MAGENDELA HAMISI
SHIRIKA lisilo la kiserikali linalopinga linalopinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake, wanaume na watoto (TAWIDO) limetoa wito kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya marekebisho ya sheria ili kudhibiti vitendo vya ukatili vinavyoendelea kushamili kwenye jamii.
Pia imetoa wito kwa Mahakama kumaliza kesi za ukatili kwa haraka na kutenda haki kwa watakaokutwa na hatia hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao ili iwe funzo kwa wengine.
Hayo yamesemwa leo Agosti 21, 2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa TAWIDO, Sophia Lugilahe, ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi habari na kusisitiza kwamba jamii kwa ujumla inatakiwa kuungana ili kufichua vitendo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria watuhumiwa.
"Kingine kinachotakiwa ni Serikali kutenga bajeti ya kushughulikia vitendo vya kikatili ili kutoa nafasi kwa watumishi wa ustawi wa jamii kuwa na fungu la kufutilia vitendo hivyo.
"Wakati mwingine watumishi wa ustawi wa jamii wanapopewa taarifa za vitendo vya kikatili wanashindwa kufuatilia kutokana na kutokuwa na bajeti na kusababisha kuzorotesha harakati za kudhibiti vitendo viovu kwa jamii,"amesema.
Pia aliwashukia waandishi habari kwa kuwataka waandike na kufichua vitendo hivyo ili rahisi kuchukuliwa waharifu hatua za kisheria.
"Hata viongozi wa dini katika mahubiri yao wanatakiwa kutoa mafundisho kwa waumini wao wawe na hofu ya Mungu Jambo litakalosaidia kupunguza ama kuondoa vitendo hivyo katika jamii.
"Nao wazazi wasikwepe majukumu ya kulea watoto kwa maana ujenzi wa tabia njema inaanza kujengwa kwenye malezi na kuwapa ulinzi," amesema.
Amesema kuwa katika ofisi yao wana kituo cha kupokea taarifa za kikatili kupitia simu na tangu mwaka 2021 na mwaka huu wameweza kupokea taarifa za vitendo vya ukatili 38, 238.
Katika takwimu hiyo, wanawake ni 27,828 wanaume 9352 na watoto ni 9038 na kuweka wazi taarifa hizo ni kwa wale wanofahamu namba ya kituoni hapo.
Amesema kuwa takwimu hizo zinaonesha jamii haiko salama Jambo ambalo litasababisha kuwepo kutokuwepo kwa maendeleo kutokana na uwezo kundi la watoto waliolawitiwa ama kubakwa , hivyo hatua za haraka zinatakiwa kuchukuliwa kudhibiti hayo.
Pia amesema katika kipindi hicho ukatili wa kimwili zilikuwa na matukio 12,243 huku ukatili wa kihusia ukiwa 7403, wa kingono ukiwa 13,216 wa kiuchumi ukiwa 3,375 na watoto ni 938.





No comments:
Post a Comment