NA BEATUS MAGANJA
MTANGAZAJI nguli, aliyekuwa akitangaza kipindi cha Dira ya Dunia katika Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Salim Kikeke amesema uwepo wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA) katika Tamasha la Kizimkazi, Zanzibar imekuwa kivutio kikubwa kwa watalii.
Ameongeza kuwa pia imekuwa chachu ya kuchagiza na kulipa hadhi tamasha Hilo kutoka taasisi hiyo kupeleka Wanyamapori hai nao wamekuwa kivutio kikubwa kwa watalii wanaotembelea Banda la Maliasili na Utalii.
Kikeke ambayo kwa sasa anafanyakazi katika kituo cha Crown FM na TV amesema hayo leo, Agosti 21, 2024 alipotembelea banda hilo na kufika katika bustani ya qanyamapori hai na kuona Simba, Chuo, Chatu, Pundamilia, Spishi za aina tofauti za ndege nyuni.
"Niko hapa Kizimkazi kwa ajili ya Tamasha la Kizimkazi na nimefurahi sana kutembelea banda hili la TAWA...kuna mabanda mengi sana lakini TAWA wameweza kuleta kivutio cha kipekee kabisa, wameleta wanyama mbalimbali na zaidi ni kuonesha hazina ya Taifa letu" amesema
"Nadhani kitu TAWA wanakifanya ni muhimu sana kuweza kuja kutoa elimu na kufahamisha jamii yetu ya hapa hapa nyumbani lakini vilevile watu wanaotoka nje ya Taifa letu kufahamu maana halisi ya wanyama hawa, jinsi tunavyowatunza na jinsi wanavyolisaidia Taifa letu kwa njia ya kipato kwahiyo pongezi nyingi sana kwa TAWA kwa kile wanachokifanya uwepo wao nadhani umeongeza ile hadhi ya Kizimkazi" ameongeza na kusisitiza Kikeke
TAWA ni mojawapo ya Taasisi za Serikali zinazoshiriki katika Tamasha hilo kwa lengo la kutangaza fursa za utalii zilizopo katika maeneo yake ya kimkakati yaliyo chini ya usimamizi wake hususani ya ukanda wa Kusini Mashariki Kama vile Hifadhi za Selous, Kilwa, Pande (Dar es Salaam), Wamimbiki (Pwani/Morogoro) n.k ikiwa ni muendelezo wa kuunga mkono jitahada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alipotangaza vivutio vya Utalii wa nchi yetu kupitia filamu Maarufu za Tanzania The Royal Tour na Amazing Tanzania.





No comments:
Post a Comment