BUTIKU AWATAKA VIONGOZI VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUWAJIBIKA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, September 10, 2024

BUTIKU AWATAKA VIONGOZI VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUWAJIBIKA


NA MWANDISHI WETU


VIONGOZI wa vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa, wametakiwa kuwajibika wenyewe pasipo kusubiri maelekezo kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  kutokana na vitendo vya watu kuuawa, kutekwa na kulawitiwa vinavyoendelea nchini. 


Hayo amebainishwa leo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.


BUTIKU alifafanua kuwa  viongozi hao wasiseme hawawajui watu wanafanya vitendo hivyo. 


"Rais amewateua kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi na mali zao hivyo hivyo na juzi amezungumza mengi kuhusu Taifa hili nadhani wangewajibika maana hawezi kufukuza kila mtu na haya yanayotokea wasiseme hawajui wanajua.... " amesema. 


Ameongeza kuwa matendo ya aina hii yaliwahi kutokea siku za nyuma na wakati wa Mwalimu Nyerere viongozi wajiuzuru ambapo Sasa wanasubiri maelekezo ya Rais na si kuwajibika wenyewe Kwa nafasi zao.


"Haya mauaji hayafai wakati umefika bila kujali vyama vya siasa, tusaidie nchi na Rais anawasaidizi wake katika maeneo husika hivyo yanapotokea hayo wanatakiwa kuwajibika," amesisitiza.

No comments:

Post a Comment